Kuna manzi kaniambukiza Yutiai aisee!
Yutiai sio ugonjwa wa zinaa masta!
Eeh nyie madokta mnatuchanganya sasa.
Wewe ndo unajichanganya hakuna Dokta alikwambia Yutiai ni ugonjwa wa zinaa!
mmm! Madokta wa siku hizi mnazingua sasa hii Yutiai nimeitoa wapi?
Inaitwa U.T.I, au Urinary Tract infection. Maana yake ni maambukizi ya kwenye njia ya mkojo. Sasa njia ya mkojo na zinaa wapi na wapi? Kwani hiyo ndude yako unaingiza kwenye njia ya mkojo?
Fanya usafi wa nyeti zako.
Epuka vyoo vichafu vya jumuiya.
Fua nguo za ndani, usivae kwa muda mrefu.
Usiku mwema!
Dr. Chris Cyrilo.