Nimepaliwa na kifupa cha samaki

Nimepaliwa na kifupa cha samaki

protonVP

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
7
Reaction score
0
Wadau,

Naombe mnisaidie namna ya kutoa kifupa cha samaki kooni. Nimekula samaki, sasa kifupa kinakwaruza kooni noma.
 
Maana yake ni nini.........?.........au sio siasa hii..........
mwaka huu nitashuhudia mengi wallah............
 
Mmh...! kama hakijatoka bado nenda kituo cha afya cha karibu watauvuta na koleo.
 
shushia wota (hot) kama ni kijfupa kidogo ila kama ni kikubwa jiingize vidole kooni then utatapika
 
Hilo ni suala la kushughulikiwa na mtaalamu wa ENT. Usikubali ushauri wa wasio wataalamu. Nenda hospital yoyote jirani watakushauri.
 
Vipi umejaribu njia ulizoshauriwa? zote ni njia sahihi maana sisi wakati tunakuwa njia ya tonge la ugali mkavu bila mchuzi ndo ilikuwa inaokoa maisha ya watu waliokuwa wanakwamwa na mifupa
 
Ukikabwa na mfupa wa samaki.........unawezaje kupata nguvu ya kupost JF.........?.........
 
Hapa kuna vitu viwili kwa Samaki
Mfupa,au Mwiba,licha ya kwamba vyote watu wanaita mfupa

Ila ungeweka wazi kama ni Mfupa au Mwiba.

Ila kama ni mfupa nakuomba nenda Hospitali
Kama ni Mwiba basi tumie njia hizo hapo juu

Sitaki kukutisha ila mie Mtoto wa Mwanzo wa Dada yangu alikufa kwa tatizo hilo baada ya kuzembea kwa wiki nzima hadi usaha ukaanza kujaa shingoni,na kufanyiwa operation akafariki at age of 20yrs
 
You're not serious...yani hadi umepata nguvu za kuanzisha uzi?,,
 
meza tonge la ugali mgumu kavukavu, maana ndio huduma ya kwanza hiyo na pia ni njia asili ya kujitibu kama umekabwa na mfupa.
 
zaman watu walikuwa wanapigwa ngumu mgongon,,wakidai inasaidia cjui ya kwel hayo,,unaweza jrb
 
Back
Top Bottom