Halafu mkiwepo hapa JF mnalalamika ooh Tz asilimia zaidi ya 73 ni illiterate wakati walimu wote mnataka muishie Dar!!Usiogope ndugu maisha huwa tunaanzia popote then ukishaimarika ndiyo unachagua pakuishi!Mimi ni mfanyakazi wa wizarani nipo Mtwara nakaribia kufa kwa kitambi kunizidia,nilipopangiwa huku wenzangu wa dar walinicheka lakini cha ajabu kila weekend wao ndiyo wa kwanza kunipigia simu kama nimeshafika dar nikawalipie bili za gambe!!Dar kila biashara ipo utafanyanini kipya utoke?nenda huko walipolala ukawaamshe nakuapia hautatamani kurudi dar kamwe!Mshahara wenyewe wa mwalimu wa serikali Dar utakusaidiaje?