Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Habari za mchana nyote,
Wlio kwenye mfungo swaumu njema inshallah mkipata thawabu mtupunguzie na sie.
Naanza sasa..............................
Kasie mie bwana nimepata jiko, jiko lenyewe ni la gesi. Kama kawaida ya Kasie hapa ndo sebleni, ndo jikoni , ndo chumbani, ndo dining, ndo maliwato basi kila kitu ni hapahapa..... ukiita kajambanane hujaenda mbali sana.
Sasa bana hadi nakuja kuelezea hili jiko ni baada ya kulitumia na kuona mambo yake yalivyo matamu...........!! Natamani na nyie mpate jiko kama hili langu ila maana chakula chake ni kitamu balaa.
Hili jiko la gesi kwanza nnacholipendea lina moto mkali pia naweza kupunguza moto iwapo ntaona moto umezidi na nahitaji moto wa taratibu hivyo mapishi yangu kutoka swaafii.
Jiko la gesi hili nililonalo ni automatic hivyo situmii kibiriti kuliwasha, nikiminya kitufe na kuzungusha baasi moto huo.
Liko fast, mradi tuu niwe nimejiandaa na mahitaji yangu yote.
Hili jiko pia lina oven hivyo nikitaka ku bake chochote au ku grill basi naweza fanya hivyo na chakula chake ni kitamu balaa. Jiko hili halijanitupa mkono wala kuniangusha.
Nikimaliza kupika ni kuminya kitufe tena na kugeuza basi moto unazima dakika hiyo hiyo.
Moto unatoka msafi hauna moshi wala hautoi masizi hivo masufuria yangu yanakuwa safii hayana masizi kabisaa.
Uzuri mwingine ninaoufurahia wa jiko la gesi ni jinsi gesi inavotoka kwenye mtungi hadi kwenye jiko, gesi haiwezi kutoka kwenye mtungi hadi nifungulie koki ya kuruhusu gesi itoke kwenye mtungi na kwenda kwenye jiko. Nafurahia sana kupikia na jiko la gesi maana hata gesi ikiisha napiga simu tuu basi ndani ya dakika 15 hadi 20 naletewa gesi hadi mlangoni, nabadilishiwa mtungi na hapo hap naendelea na mapishi.
Kabla sijaanza kutumia jiko la gesi mwanzoni nilikuwa natumia jiko la umeme, lilikuwa na utamu wake ila lina karaha ambazo jiko la gesi halina.
Umeme ukikatika sipati huduma na siwezi kupika. Kama nimetoka kazini na njaa na nataka kupika hata mayai fasta ili nipunguze njaa basi jiko hupata moto taaraatibuuu..... yaani hadi machozi yanataka kunilenga lenga...... sasa hapo utasubiri hadi kikaangio kipate moto ndo yai lianze kuiva.
Haya kwa sie tunaotunza nishati karaha nyingine ya jiko la umeme ni ukimliza kupika na ukazima jiko, basi jiko lile halipoi hapo hapo kana kwamba akitokea mtoto haraka haraka na kudondokea jikoni basi ataungua...........
Kabla sijaingia kwenye jiko la umeme nilikuwa natumia mkaa, hapa ndo kabisaaa, kwanza masizi kila mahali kuanzia kwenye vitambaa vya jikoni hadi masufuria na vyombo vingine vya jikoni. Haya ukiweka mkaa kama unapika maharage au mboga mbili basi itakulazimu ushushe sufuria chini na uongeze mkaa. Hichi kitu nilikuwa nakichukia mnooo. Halafu ilikuwa siku ukiuziwa mkaa mbichi au ambao haujakauka vizuri basi utapika chakula huku moshi unakuwakia fu fu fu keroooo.
Kabla sijatumia jiko la mkaa nilikuwa natumia jiko la mchina looh hapa ilikuwa matatizo, mara mafuta ya taa yaishe, mata tambi zimeisha, ukiwa unasonga ugalikama hujashika vizuri utashangaa kajiko kamedondoka chini na sufuria yako chinii. Ukilizima jiko huo moshi na gesi inayotoka hapo laah ni balaa. Saa ingine ilikuwa hadi namaliza kupika hamu ya kula chakula imeisha.
Mwisho wa yote jiko la gesi bana aaaah huku sibanduki labda ije teknolojia mpya ya wireless cooking heehehhehehe
All in all Kasie mie napenda kupika na jiko lngu nnavolipenda hili la gesi nikimaliza kupika nalifuta vizuriiii na kuliacha likiwa safii tayari kwa mapishi ya wakati mwingine. Jinsi nilivyo na wivu, aaah sitaki mtu mwingie atumie jiko langu maana anaweza niibia au nipokonya jiko langu. Kwa hapo wacha niwe mchoyo tuu sharing is caring but not on my gas cooker looh
Kasie nimepata jiko la gesi kwa raha na starehe zangu.
Kasie.