UONGO MWIKO
Member
- Aug 31, 2011
- 20
- 5
Usiende mkoani, baki Dar.
Kombo usidanganye watu bwana, jina lako laonesha Dar es Salaam ni kwako au watoka jirani na hapo. Waache watu wakalete maendeleo nje ya Dar.Usiende mkoani, baki Dar.
Bora ubaki tu hapa hapa, huko meatu porini hata ukiwa na gari utatembea nalo wapi.
kama kule kuna san siro,maisha club,bahari na mihuri ya mifukoni nenda na kama foleni za magari,ukosefu wa maji,umeme na mazingira machafu ya dsm havikuathili baki.mia
Wenye akili mgando, wasiojiamini, washamba, waendekeza starehe za kulala club, na wasiokuwa na malengo katika maisha yao ndio wanang'ang'ania kufanya kazi Dar es salaam. Utakuta mtu anapata kipato kidogo, ila kwa kuwa yupo tu Dar anaridhika ile mbaya, utadhani mwanamuziki wa Bongo Flavour au akina Majuto wasiokuwa na profession ya kuwalipa mikoani.
Nani kakwambia mshahara utakuletea maisha bora? Hata ukawe Mkurugenzi wa TANROAD mshahara haukutoi ng'o. Hiyo ni mbegu unayotakiwa uipande. Lakini utaipandaje mbegu Dar es Salaam ambapo kama wataka kufungua biashara bei ya pango la frame ni sawa na mshahara wako? Kaangalie watu waliotengeneza pesa wametokea wapi kabla hawajafika Dar es Salaam. Wengi wametoka mikoani, tena sio makao makuu ya mikoa bali mawilayani kabisa. Nimesikia kuna watu wakienda Mbarali au huko Kamsamba Sumbawanga yaani hawarudi wakilikamata jembe. Dsm ina wenyewe, kama akina Manji. Akina sisi tukikaa Dar tutaishia kutamani tu wenzetu mafisadi wanapo invest na pia kufurahia foleni na mataa ya usiku.
Ukienda mkoani wala huatatamani kurudi tena dar.
Mkuu nenda mikoani kuna fursa nyingi za kiuchumi mambo ya kuganda Dar ni ushuzii mtupu hakuna lolote la maana zaidi ya joto kali,foleni,starehe za kijinga,.
watu kama nyie ndio huwa nawashangaa sana...nenda kapige kazi huko pia ni tanzania. hivi unadhani kila mtu akikataa kwenda kufanya kazi ma-wilayani ni nani atakaye wasaidia wananchi wa sehemu hizo? halafu ukienda huko ni namna nyingine ya kujifunza na kufahamu nchi yako ilivyo hasa maisha ya mikoani. sidhani kama ni busara kwa kila mtu kung'ang'ania hapa dsm.tatizo nashindwa kuelewa kwa nn moyo wangu umekua mzito..........sijafanya maamuz nna siku 3 sasa..sina sababu za msingi saana zaidi ya mchumba ambaye yy analia tu mda wte akiskia naondoka,halinipi shida sana......sasa nitaufahamu vp huo mji?nitakua pia hadi maswa...nahitaji kufahamishwa na wenyej plz