Nimepata mil 10 ghafla, nataka ninunue mchele kisha niuze mwezi 10. Je, kuna zao lingine bora zaidi?

MORIAH

Senior Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
103
Reaction score
51
Wadau ktk muda ambao sikutarajia nimepata mil 10 kutokana na mikopo kwa wafanyakazi niliopewa na benki yangu kama mfanyakazi - sikutegemea kabisa japo nilikuwa natafuta fedha hizi muda mrefu.
Sasa nataka niende Morogoro ninunue mchele kisha niweke ktk Godown halafu nitauza bei ikipanda. Kwa sasa ndo wazo nililo nalo. Je, kuna mtu mwenye wazo bora kuliko hilo? Au je biashara hii ina changamoto gani?

Je, huko kwenye godown kuko salama?
Je, hakuna uwezekano wa bei kutopanda?
Niliwahi kufanya biashara ya namna hii Upande wa Mahindi huko Arusha miaka mingi. Sina uzoefu wa mchele. Naombeni ushauri wenu.
 
Hilo godown linamilikiwa na nani?

Gharama ya usafiri toka shambani mapak kwenye godown na later kutoka kwenye godown mpaka kwa mteja ni sh. ngapi?

Umewahi kuongea na mtu mwenye uzoefu na huduma ya hayo magodown?

Kwa sababu pesa umeshachukua maana yake ni kwamba tayari umeshaingia kwenye deni, kwahiyo inabidi ufanye hesabu interest rate ni sh. ngapi ili usije kujikuta unaifanyia kazi bank.
 
changia 1,000,000 JF, zilizobaki fanya biashara unayokusudia utafanikiwa sana.
 



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Swali lako ni zuri sana.. Mi nakushahuri iyo hela husiitupe yote kwenye mradi mmoja ila uangalie na ishu nyingine za kufanya.

Maadamu umekopa kama mfanyakazi najua utalipa deni ila kwa kweli bado kuna umuhimu wa kuangalia njia sahihi ili mwisho wa cku biashara utakayoifanya ifidie kile unachokitoa kwenye mshahara wako.

Mi sina idea mbadala ila ninajaribu kukupa msisitizo ili husifanye makosa ukaja kujuta. Swala la interest rate nalo ni jambo la msingi husijepiga hesabu ya Mil 10 tu!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu naomba kuchangia kidogo...

Kwa kuwa una GODOWN tayari Ukitaka faida kubwa kwenye biashara ya mchele ni bora ukanunua mpunga toka pale IFAKARA ukauhifadhi mpaka msimu chakula kikiisha mashambani ukawa unaukoboa kidogo kidogo mwenyewe unaingiza sokoni..faida huwa ni kubwa mno ukilinganisha na mtu anayenunua mchele na kuuza mchele..
Ukinunua mchele na kuuza unakua huna tofauti na mchuuzi wa biashara ya maji anayetembea kutwa nzima na maji ya chupa wakati faida ni tsh 30 hadi 100 kwa chupa moja wakati huo huo barekhsa anaingiza tsh 300 kwa chupa moja ya maji.

Maeneo mazuri ya kupata mpunga mzuri wa BIASHARA kama una usafiri mzuri ni IFAKARA kama unaelekea MAHENGE ukishavuka tu mto KILOMBERO kama unatokea IFAKARA MJINI uliza eneo moja wanaita MASHAMBANI, ni maarufu sana wenyeji watakuelekeza... Kawaida ya biashara ya kununua mpunga kuukoboa na kuuza ,SHILLINGI inazaa shillingi so kama utachukua mzigo say wa million 7 tegemea kupata millioni 14 mwisho wa msimu... Ukishamaliza mzigo woote tafuta tena mazao mengine yaliyo katika msimu huo basically alizeti ..usiache fedha ikakaa idle ukisubiri msimu mwingine(hiyo ndio siri ya biashara ya mazao)..

Wazo lako ni zuri sana, Fanya hivo mkuu usife moyo mkuu, asilimia kubwa ya watu wasio na entrepreneurship spirit(wanaopenda kazi za kulipwa mishahara mwisho wa mwezi) ni wazuri sana katika analysis hasa za hasara na kukatika mtaji lakini ni ZERO katika ACTIONS. Ukiwasikiliza sana utakufa masikini ukisubiria kiinua mgongo cha JK...
 
Asigwa amekuelekeza vizuri sana, ila fanya utafiti wa ufuta pia unalipa vizuri sana na itakubidi uwe na mtandao wa wakulima bila kuwasahau watendaji wa vijiji watakusaidia sana inakubidi ujitambulishe kabisa na kutafuta kijiurafiki.
 
Kama alivyosema asigwa ni bora ukahifadhi mpunga badala ya mchele, kwani ukihifadhi mchele kuna uwezekano mkubwa sana ukaharibika kabla haujauuza.

Vilevile biashara ya mazao inahitaji committment na muda wa kutosha kwani unakwenda kuitafuta mashambani na si kwamba huo mpunga utaupata kwa siku moja. Itakuchukua si chini ya wiki mbili kuweza kukusanya gunia 100. Kwa hiyo jitahidi kutenga muda au uwe na mtu ambaye yuko committed na ni mwaminifu kuweza kufanya kazi hiyo.

Kuhusu faida nina hakika ni nzuri sana, na soko la chakula siku zote halikosekani hasa katika kipindi cha kilimo. Nina hakika pia msimu wa mwaka huu kutakuwa na uhaba wa chakula kwa sababu mvua hazikunyesha kwa wakati katika maeneo mengi, hivyo mavuno hayatakuwa mazuri na bei ya chakula itakuwa juu hapo baadae. Wakati mwingine unaweza kujikuta unawauzia hao hao waliokuuzia na still ukapata faida nzuri tu.
 
<br />
<br />
Kwenye mradi wowote kitu cha samani zaidi ni muda,shilingi 1 moja utakayoingiza leo thamani yake ni kubwa kuliko shillingi 1 hiyohiyo utakayopata kesho,.......biashara ya mazao in rsiks nyingi,na siku zote biashara yenye risks nyingi na returns zake ni nyingi pia,kwa hiyo hii ni biashara sahihi,sasa binafsi siamini sana ktk biashara ya kununua kitu (ni similar to ulanguzi)na kusubiri hadi bei ipande ,kufanya hivyo kunasababishwa na woga,trade unproffessionalisim na greedy,muda huu wakati umeweka mzigo ndani unapunguza mzunguko wa pesa(that 10 m of yours)...unapofanya hii biashara kwa msaada wa vyombo vya habari utambue maeneo yenye uhaba wa bidhaa hiyo,mfano kando ya kaskazini inaweza isiwe na upungufu while kanda nyingine ina upungufu na kupuleka huko sio kuweka ghalani hiyo biashara ya kizamani,afu nchi yetu inafursa kubwa waweza kutafuta fursa hadi ktk nchi jirani,all ze best I hope to hear your successes here very soon.
 
Nafanya biashara hii, mwaka jana niliwekeza kwenye mchele wa kiasi cha milioni 40..nikitegemea nisubiri bei ipande niweze kupata faida nzuri tu...lakini matokeo yake serikali imeruhusu mchele wa bei rahisi toka nje..imekula kwangu..mchele upo kwenye godown mpaka leo hii..siwezi uza kwa hasara......so be forwarned!!!! kama ni wazo lingine la biashara you might just pm me so that we can discuss
 
Kipindi hichi sii cha kununua mazao ni mpaka july!nenda kawakopeshe wakulima sh 40,000 kwa gunia la mpunga july wakivuna, ambapo hapo hapo shambani utauza gunia sh 80,000
 
m 10 unafungua thread jf
ukipata mia si tutakuzika jamani?
 
m 10 unafungua thread jf
ukipata mia si tutakuzika jamani?
bibie nimecheka sina hamu,huoni anasema amepata ghafla utafikiri kaokota au kapewa rushwa kumbe mkopo,atakatwa salari mpaka astaafu tena kama ni barclays mkopo hautajakaa uishe
 
Kipindi hichi sii cha kununua mazao ni mpaka july!nenda kawakopeshe wakulima sh 40,000 kwa gunia la mpunga july wakivuna, ambapo hapo hapo shambani utauza gunia sh 80,000
Hiyo ni risky sana. kama hakuna mavuno ndio nitolee hiyo.
 
m 10 unafungua thread jf
ukipata mia si tutakuzika jamani?
Binti usimkatishe tamaa mwenzio. Milioni kumi ni nyingi sana kama akitulia na kubuni njia ya kuzizalisha. Kuna watu sasa ni matajiri na walianza na pesa ambayo thamani yake ni chini ya hiyo 10M ya sasa.
 
Binti usimkatishe tamaa mwenzio. Milioni kumi ni nyingi sana kama akitulia na kubuni njia ya kuzizalisha. Kuna watu sasa ni matajiri na walianza na pesa ambayo thamani yake ni chini ya hiyo 10M ya sasa.

Ndio maana watanzania wengi hatuendelei ni masikini kwa ajili ya kukatishana tamaa kama hivi badala ya kupeana moyo.
 
Ndio maana watanzania wengi hatuendelei ni masikini kwa ajili ya kukatishana tamaa kama hivi badala ya kupeana moyo.
Usikute yeye mwenyewe hajawahi kushika hata 500K ya kwake mwenyewe. Anyway nisiseme sana pengine ni utoto tu. Akija kupata majukumu atajutia kejeli zake.
 
Usikute yeye mwenyewe hajawahi kushika hata 500K ya kwake mwenyewe. Anyway nisiseme sana pengine ni utoto tu. Akija kupata majukumu atajutia kejeli zake.

Kweli bora tukae kimya tusijeingia kwenye mtego huo huo..
 
Marejesho ya mwezi unarejesha kiasi gani? Unarejesha kwa muda gani? Unaishi wapi? Jinsia gani? Dini gani? Unapenda nini? Unaishi na nani? Umeoa ama kuolewa? Kama hutojali nijibu maswali hayo nikupe ushauri, maana biashara hutegemea mtu na mtu pamoja na hayo niliyokuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…