Mkuu sipo pole sana kwa msiba. Msiba uko wapi? Tupo pamoja kwa sala katika kipindi hichi kigumu, naamini Mungu atakupa nguvu na Hekima ya kumaliza salama.
pole sana, jipe moyo ukamilishe shughuli za msiba na uwe jasiri ili kuendelea na maisha, kila mmoja wetu anayo siku yake, hivyo hiyo ndo njia yetu sote.
Pole sana mkuu, Mungu akupe nguvu hekima na busara ili uweze kuomboleza na baadae kusahau kwani ukizidi kuendelea kukumbuka hautapata nguvu ya kufanya lolote tena. Tuko pamoja mkuu japo sio kimwili bali kiroho tupo pamoja.