Ndugu wana JF nashukuru sana kwa sapoti yenu, nadiriki kusema kuwa mmekuwa sehemu ya familia yangu kwa kiasi ambacho siwezi kukisemea hata kwa chembe ya maneno au kuitenda kwa jinsi yoyote ile kwa aina yoyote ya matendo. Nashukuru kuwa maombi na sala zenu zimetuwezesha kufika salama Arusha ingawa bado wengine wanasafiri ila ni imani yangu kuwa watafika salama wote pia.
Maziko yatafanyika Jumatatu ya tarehe 26/11/09 kijijini kwetu, hii imetokana na Dayosisi ya Mkoani Arusha kuomba nafasi ya kushiriki kwa kila hali kutokana na Marehemu Babu kuwa mtumishi wao kama Mchungaji kwa kipindi kirefu tu.
Hali ya huku kwa sasa ni mvua sasa kwa hizi local roads kunatokea matatizo ya hapa na pale lakini ndio barabara zetu tutamaliza kwa amani tu ndio imani yetu.
Nashukuru tena sana ndugu zangu "Be blessed all"