Sio rahisi kama unavyofikiri,kumbuka tupo Tanzania nchi ambayo tu masikini(ila mafisadi ni matajiri) kwani basic needs za mtoto unayesema ni rahisi kumlea kuzipata ni ngumu labda uwahakikishie wana jf u fisadi pia.
Hongera sana Mzee fanya mambo urudi nyumbani ukamuone mwanao!
Hongera sana mkuu kiss the lil angel for me plz
.......Congrats for u and your wife
mkuu hongera sana! mwenzio baada ya kumpata kelvn niliahidi sitafunga mdomo wangu see my avatar!
I CAN FEEL UR FURAHA YA KO MKUU!
hapa natetemeka kwa furaha, nimeweka muziki wa rose mhando uitwao MUNGU NITAKUSHUKURU. nimejawa na furaha, lakini niko mbali sana nje ya Tanzania, ningependa kuwepo lakini nimesafiri masafa marefu kutafuta maisha lakini mwenzangu kwa ujasiri mwingi kajifungua salama mtoto wa kiume! Glori to God.
nimetafuta kila upande ndugu yangu wa kumshirikisha furaha yangu nimekosa isipokuwa JF members. jamani Mungu ashukuriwe kwa jinsi anavyotujalia waja wake mapaji kwa ukarimu. libarikiwe jina la Bwana wa Mabwana. amen.
nachakarika nirudi mapema nyumbani kumpakata mwanangu... ooo, nimejawa na furaha wapendwa siwezi kusema kwa usahihi
Utangulizi
ee Mungu wangu nitakushukuru,
mbele ya mataifa yote nitaimba,
dunia nzima nayo itambuliwe hilo,
kwamba jina la Yesu pekee ndilo,
ulimwengu mzima uokolewe kwalo,
1.
asubuhi na mapema, mimi nitaimba,
kabla ya kinywa kunena, kwako nitaimba,
jua lijapozidi, kwako nitaimba,
nijapoteswa kabisa, kwako nitaimba,
nijapodharauliwa, kwako nitaimba,
kiitikio
swii swii swii swiii sikia ee kinanda,
swii swii swiii swiii amka ee kinubi, x2
inuka ee zomari imba kwa sauti,
wo wo wo wo atukuzwe Mungu, x2
ye ye ye ye Jehova Adonai x2,
El Ghibor Shalom, Mungu unayejibu
El Ghibor Shalom, Mungu unaitika
uniondolee majivuno, komesha kiburi
utawale akili zangu, Bwana niongoze,
uifundishe roho yangu, habari za mbingu,
sikizeni ee kizazi changu, Mungu anaishi x2
2. nipe moyo wa nyama, uliopondeka,
moyo ulotulia, na myenyekevu,
mimi si kItu kwako, ni mdudu tu,
mimi ni kama nani, uniinue,
unifinyange Bwana, kama upendavyo,
unifundishe Bwana, kama upendavyo..
kiitikio
swi swi swi swi….
ndugu yangu hata pumzi zinakaribia kuniishia, looooh!! God is good。
asanteni wote jamani kwa pongezi na dua. kwa taarifa tu ni kwamba sasa wameisharudi nyumbani wanajichana mitori na supu tu kwa kwenda mbele! jamani mambo mengine raha sana jamani nyie acha tu!
miss Judith nashukuru kuungana nami kwa kutuwekea music halisi unaonikonga moyo wangu sasa hivi. ni kweli ndio huohuo.
jamani, acheni Mungu aitwe Mungu!