Nimepata soft loan bila riba

akanunue symbion/dowans awasaidie tanesco manake mgao ushakuwa kimeo
 
Hizo ni pesa chafu na kama alivyodokeza Mwalwisi ziko punishable against "anti- money laundering act". Ole wake yeyote atakayekutwa nazo. Dubai kuna Wa Pakistani na Wa Afghanistan wanauza magari kwa bei ya kutupa na lengo ni kusafisha fedha za dawa za cocaine na silaha
 
Mkuu, mimi takufanyia miundombinu takupeleka Kwa Gavana Beno Nduru upate kibali cha kununua Dola, paundi, then unatafuta place pale mtaa wa Samora unafungua Bureau de Change, upo tayari tufanye kazi?
 
Mkuu, Dubai sehemu gani? Kama vipi ni-PM
 
Hiyo hela unaweka bond (security) kitu gani ? Au ni unsecured loan ? What if ukishindwa kurudisha ndani ya huo muda ? What if ukichukua huo mkopo (kama ni unsecured loan) ukasepa kimya kimya ? Isije kuwa hizo hela unaweka rehani maisha yako.

Sio rahisi katika mazingira ya kawaida hapa duniani mtu akaanza kwa kukupa bilioni then akategemea uirudishe ndani ya miezi miwili, unless uwe tayari una biashara, au tender au project ambayo inarun na unahitaji cash ya kuiboost. Kuestablish biashara mpaka isettle within huo muda na kupata hao wateja si kazi ndogo. Vinginevyo hiyo biashara iwe ni ya magendo.
 
Chukuwa hela, nunua bonge la bangalow/office kama 3 au 4 hivi ukapangishe kwa NGO wakulipe kwa mwaka wote....
 

Mkuu koboko/nyoka sorry naomba nitoke nje kdg ya mada. Jana nilikuwa Arusha looks like hawa jamaa wa Bamburi wanataka kudominate soko la saruijii Arusha na sasa nasikia tena kutoka kwako Mwanza. Hv tatizo ni nini hasa kwamba saruji yetu bei iko juui, ubora uko chini au haitoshelezi? Ninaboreka sana kwamba nafasi za ajira nchini ziko chache sasa tunapoanza kuziexport hata zile chache zilizopo napata hofu kidogo ya future ya watanzania.
 
hapo pekundu.unataka hadi aandike riba ya 15% no ujue ni riba??
sasa ulikopaje hela bila kujua utafanyia nini??
me na doubt huo uwezo wa huyo jamaa kukopesha!!

Mkuu ingawa technically na hii anayotoa hapa ni riba (lakini this is profit interest) tofauti na interest za mkopo ambapo unarudisha pesa ulizokopa na percentage ya pesa ulizokopa regardless umetengeneza faida au la...

Lakini case ya huyu bwana ni kwamba atampa 15% ya faida atakayotengeneza kwahiyo akipata faida ya tshs 100 atampa tshs 15; akipata hasara atamrudishia pesa yake aliyokupa bila riba.

Kwahiyo way out achukue 1bn atumie hata 5m apate faida hata ya 3m alafu amdanganye jamaa alifanya biashara ya kukopesha watu deal zikaharibika na watu hawajamlipa so here is your 1bn
 

well said voice of reason, watu walikua hawajamuelewa hapo.
 
Dah, ina maana ushachukua mzigo? Chukua kaziweke bank baada ya miezi miwili utapata kafaida, ukimpa mwenye pesa 15% ya faida yako I am sure utabakiwa na chochote cha maana. Kumbuka bank ni safe sana kama hizo pesa zenu ni halali.
 
Hiyo transaction ya 1-3b, in cash.....
Hapana.....

 
Hela londadi hiyo itakupeleka jela.
 
Blue balaa nasikitika umepata fursa ya kukopa kabla hujajipanga siku nyingine fanya utafiti wa biashara gani ya kufanya kabla hujaenda kukopa otherwise watu watakushangaa hata huyo aliyekupa nafasi kukopesha akiona muda mwingi hujaenda kukopa anaweza kuruka
 
RR Wapi utapata riba ya zaidi ya 15% benki kwa miezi 2 labda afanye biashara ya kununua na kuuza dhahabu
 

Hiyo ya Cement kaka imekaa vizuri, tatizo Kuna Wanaweka mpaka $m nyingi sana pale, yeye anakidai kiwanda!!! Pale Mwanza kuna wakina Lameck wamedominate sana soko hilo; na wana influence na Viwanda vya Kenya-wameweka pesa nyingi mno.
Kwa nini huyo jamaa anataka pesa ya fastafasta? Hesabu za huyo jamaa na pesa yake zinatia mashaka.
 

Huenda wewe unaacsess na pesa za BOT (and the like), sas unataka kuzifanyia mambo ya DECI! Ogopa sana mkubwa.
 

mkuu hata mimi nashangaa, but ni eona simba cement wamefungua kiwanda chao kipya kule kenya, si jajua wana means nini hasa
 
Too good to be true
 
Nina wasiwasi kwamba zinaweza kuwa PESA ZA BANK na kwa kipindi kifupi, wanachota na kukopesha. Muda ukifika, wanazirudisha na faida yao juu. Tatizo ni ukichukua na ukapotea nazo. Sijui wanatumia vigezo gani kwenye kukopesha ili mtu asipotee (Bima) na pesa.

Hiki kipindi ni kifupi sana. Labda ni kwa wale ambao mzigo umefika na hana pesa ya kuutowa mzigo. Anachukua pesa, anatoa na kuuza na kurudisha pesa za watu. All in all, hawa jamaa watakuwa na UTEMI fulani mara ukishindwa kurudisha hiyo dola milioni yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…