Nimepata wa kunifadhili masomo yangu, lakini kuna hili

Raelish

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
489
Reaction score
162
Aman iwe kwenu wapendwa,

maisha yapo kasi sana na kila hatua ina maana km sio kwako moja kwa moja basi kwa jiran yako., ok ngoja niend kt point yang,baada ya kuzunguk sn kutafut mfadhl wa masomo yang hatmay nimefanikiwa.,

kuna mtu amejtokez kunisaidia lakn yey ana kpato cha kawaid, kaz yake ni uuguz(murse). Ameniambia yupo tayr kunsaidia ila hana uwez wa kulp gharama za chuo kwa awam 2 bal amenpa options 2..

ya kwanz niend chuon nikaomb gharama zgawanyw kwa mwez(miezi) alaf yey azlpe kwa mwez mpk gharam za mwak znaisha, ya pili nitaft mtu aliye tayr kuniazm pesa ht 1.5mil hv alaf yey atarejesha kwa kadri ya makbaliano.

Ile njia ya kwanz imekuw ngum kdg, hii ya pili nimeon nije kuwashrksha ndugu zangu hapa km kun mtu anawez kuniungansha na mtu au taasis weny mkopo angalau weny mashart nafuu afany hvyo anisaidie, (altak akope benk lakn tayr ana mkopo mwngne benk). Nmechaguliw dip.in clinical med & dip.in pharmaceutical science.. mm nmepend clnc medcn, ada ya chuo kwa mwak ni 2.6mil. Ahsanten, nasbr msaad wakobd
 
Kuna foundation inaitwa karimjee Jivanjee Foundation inatoa sponsorship ebu fuatilia uone. Itakuwa vipi!
 
Raelish ukileta shida kwenye jukwaa hili walau uandishi wako ulete picha ya kusaidika.Walau jitahidi kutofupisha maneno.
 
Nenda Halmashauri ya Nkasi wana utaratibu wa kusomesha wanafunzi kwa bond. Masharti ni kuwa ufanye kazi kwao kwa miaka kadhaa ukimaliza shule. Mtafute district health secretary wao akupe taarifa.
 
Raelish ukileta shida kwenye jukwaa hili walau uandishi wako ulete picha ya kusaidika.Walau jitahidi kutofupisha maneno.

Kwanza nisamehe sana kwa hilo, rafiki yangu mimi natumia mchina na imelimit maneno(herufi) ya kuandika yasizizi 1024 tu, hivyo habari yangu yote ifike natakiwa kufupisha maneno ili angalau iwe ndefu kidogo na ieleweke... nisamehe sana na sababu kubwa ndo hiyo mkuu
 
Tafuta vyuo vya serikali ada yake ni ndogo haitakutesa hivi...Scholarships za diploma sijawai ziona kirahisi.

nimejitahidi sana kutafuta vyuo vya serikali nimekosa ndugu yangu
 
Sijapenda aina ya uandishi wako hata kidogo.

nimekuelewa ndugu yangu,lakini nimetoa sababu juu hapo.. tusameheane ipo siku nami nitapata pc au simu itakayoniruhusu kuandika herufi nyingi hivyo sitakuwa na sababu ya kufupisha maneno
 
namuhurumia anayekusaidia kwa uandishi huu anapoteza tu hela yake
 
namuhurumia anayekusaidia kwa uandishi huu anapoteza tu hela yake

Mkuu ameshasema anatumia simu ambayo kuna limit ya maneno, amejaribu kufupisha ili yaeenee mengi angalau alichotaka kutueleza kieleweke.

Ukisoma thread soma kwanza na michango ya waliokutangulia kabla nawe hujachangia.
 
namuhurumia anayekusaidia kwa uandishi huu anapoteza tu hela yake

jaman mbona nimetoa sababu hapo juu? nijielezeje wanadamu nyie mnielewe? ni kutokana na simu ninayotumia ina nilimit niandike herufi 1024 tu, hivyo inanilazimu nifupishe maneno ili angalau nieleze kiurefu nieleweke... acha kuuchoma moyo wangu bhana.
 
Mkuu ameshasema anatumia simu ambayo kuna limit ya maneno, amejaribu kufupisha ili yaeenee mengi angalau alichotaka kutueleza kieleweke.

Ukisoma thread soma kwanza na michango ya waliokutangulia kabla nawe hujachangia.
unadhani sijasoma kaka....huyu dogo anazingua aisee...ukifuatilia posts zake zingine kwenye jukwaa la siasa anaandika vizuri tu...huku kaja kutuzingua tu
 
unadhani sijasoma kaka....huyu dogo anazingua aisee...ukifuatilia posts zake zingine kwenye jukwaa la siasa anaandika vizuri tu...huku kaja kutuzingua tu

sasa we nenda jukwaa la siasa kahesabu herufi katika thread yangu, zikizidi 1024 waambie mods wanipige ban tena iripoti hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…