JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Nilipofika hapo wameandika huduma zao zinatolewa kwa saa 24, nilimpeleka Mtoto wangu ambayo alikuwa anachemka sana, nikaamini nitapata huduma ya haraka.
Nilikuwakuta wahudumu wapo wakiwemo wale wa manesi wa mapokezi n ahata daktari pia, lakini kilichonishangaza ni kuwa waliniambia hakuna huduma ya vipimo.
Sasa nikajiuliza wao wanafanya nini muda huo kama wako hapo Saa 24 na hawana huduma ya vipimo, inamaana mgonjwa anapofika wanampaje huduma kama hawana hata mchakato wa upimaji.
Nilipohoji hivyo nikajibiwa kuwa wikiendi hasa husiku huwa hawana huduma ya kufanya vipimo, nikahoji hivyo wao wanafanya nini hapo au wanawatibu vipi wagonjwa muda wa usiku? Sikupata jibu.
Natoa wito kwa Serikali hasa Wizara ya Afya kuangalia hivi vituo vyao vidogo, kama wanatambua ni sehemu ya kupata huduma ya kwanza kabla ya kwenda hospitali kubwa, siku tatu za wikiendi kwa maana Ijumaa, Jumamosi na Jumapili usiku hakuna huduma ya vipimo, hilo ni tatizo tena tatizo kubwa.
Vituo vidogo vipewe uwezo wa kuwa na vipimo hadi usiku au kama ni uzembe wa hicho kituo hatua zichukuliwe, kwani watu wengi wanaweza kupata madhara makubwa kwa kuwa tu kituo cha karibu kama hicho hakina huduma ya upimaji.