Nimependa Vladmir Putin alivyooiita nchi yake "Fatherland". Nashauri na Tanzania tuachane na kauli za "Mama Tanzania"

Nimependa Vladmir Putin alivyooiita nchi yake "Fatherland". Nashauri na Tanzania tuachane na kauli za "Mama Tanzania"

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Kulifananisha taifa na mama ni mbinu za kisaikolijia kulivunja morali.

Sijui chanzo cha sisi Watanzania kujiita MAMA TANZANIA au MOTHER LAND BADALA YA FATHER LAND

Tumuige Putin kuiita nchi yetu BABA TANZANIA. AU TUTUMIE NENO FATHERLAND BADALA YA MOTHERLAND.

SABABU ZANGU

1: Mama ni mwanamke, na kimaandiko ya Imani za kidini na kijadi mwanamke ni kiumbe dhaifu. Hivyo kujinasibisha na mama ni kujinasibisha na udhaifu.

2: Kiasili Baba inawakilisha majukumu, ukakamavu kukomaa. Na mama inawakilisha kuletewa, kufanyiwa hata Ukifanya wewe unafanya kidogo sio mambo makubwa. Ni vigumu kummotivate mtu Kwa kutumia mama.

3: Wakati mwingi tumeaminishwa mama ni kitu Duni. Naamini sio Tanzania ni Hadi ulaya Kiasili.

Ndio maana tunamisemo kama.
"LELE MAMA"

"MTOTO WA MAMA"

"MAMBO YA KIKEKIKE"

Nini maoni yako.

URUSI NCHI YAO INATAMBULIWA KAMA FATHERLAND SIO MOTHERLAND

 
Since ancient times nchi ni feminine kind of. Nchi ni mama wa kila kitu and that's why our ancestors have been referring to lands in feminine pronouns than masculine.

Fashisti ana akili kuliko mababu na mababu wa dunia hii tangu miungu ya Uajemi hadi Mungu wa Yakobo? Nope!
 
Kwa hiyo wewe unamdharau sana mama au?
Mama simdharau namuweka sehemu yake. Mama na Baba wanacomplimentary roles kama kufuri na funguo. Ila Baba Ndiye kiongozi katika mahusiano hayo.

Hivyo kujinasibisha na Baba Kuna ongeza nguvu flani.

Pia sisi watu wa Imani tunaamini, Land alipewa Adam (baba) Kisha akaumbwa mama baadae ili wasaidiane kuitiisha na kuzalisha.
Hata mama anatokana na Baba.

Hivyo hata kuita Motherland huo msemo Bado unamgogoro.

Licha ya warusi wengi kutomuamini Mungu ila hili la Fatherland nimewaelewa sana
 
Umesema sahihi kabisa mkubwa.Hii ya kuita mama inatufanya nchi yetu iliwe na mafisadi wachache kwa kuwa wanajuwa mama siku zote hana maamuzi.mama ni mpole na ni mpishi wa mume wake baada ya mme kufanya kazi kubwa ya maendeleo
 
Motherland kwasababu inazaa.
Kuzalisha nadhani ni powerful kuliko kuzalishwa. Uzalishaji. Productivity inauhusiano mkubwa na fatherhood..
Kubadilisha jina hakubadilishi uhalisia. Kama wewe mnyonge utakua mnyonge tu hata tukikuita power Mabula.
Uhalisia huanza kubadilishwa na mindset

Ukiwa na mindset ya kimama unakuwa legevu, taifa likiwa na mindset la kibaba matendo yanabadilika.

Ndio maana wakati sisi nembo yetu ni twiga mpole Urusi ni Dubu mkali
 
Mama simdharau namuweka sehemu yake. Mama na Baba wanacomplimentary roles kama kufuri na funguo. Ila Baba Ndiye kiongozi katika mahusiano hayo.

Hivyo kujinasibisha na Baba Kuna ongeza nguvu flani.

Pia sisi watu wa Imani tunaamini, Land alipewa Adam (baba) Kisha akaumbwa mama baadae ili wasaidiane kuitiisha na kuzalisha. Hata mama anatokana na Baba.


Hivyo hata kuita Motherland huo msemo Bado unamgogoro.

Licha ya warusi wengi kutomuamini Mungu ila hili la Fatherland nimewaelewa sana
Wewe kuna kitu hukielewi vizuri, unakimbilia tu sijui imani za dini sijui mamlaka?

Nataka nikuulize swali.

Anaembeba binadamu mwilini mwake hadi anakamilika kutoka duniani ni nani?

Anayemnyonyesha kipindi hawezi kula chakula cha kawaida ni nani?

Anayemlisha na kumuogesha na kumvisha nguo ni nani?

Anayehakikisha huyo mtoto amekula ameshiba na ameenda shule ni nani?
Mtoto anafunzwa na baba au na mama?

NA ASIYEFUNZWA NA MAMAYE HUFUNZWA NA NANI?

Ndugu, kwa ustawi wa jamii na maisha ya binadamu kwa ujumla, mama ndiye anayehusika zaidi. Nchi ni kama mama, inakulea, inakulisha na inakufunza pia. Mama ni kama ardhi yenye rutuba ambayo baba yako aliweka mbegu ikastawi, Mama ni kama nchi inayostawisha watu wake.

Hizo ngedembwe na jeuri za Putin ni ulevi tu wa madaraka, na kwa sababu Putin amemkataa mama, amekataa kufunzwa na mama, soon ulimwengu unaenda kumfunza.
 
Tanzania is the land of ancestors. It is right to be called fatherland.
 
Kuna very deep philosophical meanings and explanations on why a country/ nation is called/regarded as MOTHERLAND. For those who don't know this like Putin can name their countries/nations whatever they want.
 
Putin uzee unamsumbua ilitakiwa awepo Cage ya wazee akitunzwa huko..
 
Back
Top Bottom