Habari zenu wazee wa mmu,
Nina mfanyakazi mwenzangu ambae pia ni best yangu sana kwa kuwa hata mipango ya maisha huwa tunapeana mbinu mbili tatu ili tuweze kuzidi kunyanyuka kimaendeleo.
Mimi nimeoa na yeye ameoa sasa huyu jamaa yangu ni type fulani ya watu wapole kupita kiasi.
Hapa karibuni mke wake kamfukuza dada wa kazi na mtoto na wana mtoto wa miezi 10 hivi kama sikosei,mke wake nae ni muajiriwa sector nyingine tofauti na yetu, sasa huyu jamaa yangu huwa nampitia kumchukua na tunaenda kazini kwa sababu gari yake imepata ajali haiwezi tembea. Imekuwa kama ratiba ya kawaida mimi kumpitia pale nyumbani kwake kwa kuwa ni njiani kuelekea kazini
Sasa siku moja nimepack kwa nje namsubiria jamaa akatokea dada mmoja na kunisalimia nikiwa ndani ya gari akaniomba nimpe namba yangu kuna ishu sensitive anataka kuniambia. Mwanzo nilihisi labda anataka tuanzishe mahusiano nikataka kumpa namba ya uongo anyway kwa sababu mimi ni mwanaume nikasema ngoja nimpe ya ukweli.
Siku ya pili tangu nichukue ile namba nikapokea namba mpya kumbe ni ya yule mdada akaanza kuniomba msamaha kuwa hajapenda kunihusisha mambo ambayo hayanihusu,nikamuuliza mambo yapi?
Akaanza kuniambia rafiki yako unampitiaga kila siku kuna mchezo anachezewa, kuuliza upi akasema "Kaka nyie mkiondoka mke wake huwa anampeleka nyumba ya jirani mtoto kwa mmama fulani ambae huyo mama ana kijana yake ambae huku mtaani tunajua anatembea na mke wa rafiki yako na mtoto ni wa huyo jamaa so pale kwa yule mama kuna kila aina ya vikolo kolo vya kuchezea mtoto vimenunuliwa na yule kijana wa yule mtoto na yule mama
Kwa kujiongeza nikasema isije huyu dada alikuwa na mahusiano na jamaa yangu hivyo kaachwa sasa anataka kusambaratisha ndoa ya huyu rafiki yangu ikabidi nianze kuchunguza ndipo nikapata jina la yule kijana wa yule mama na kulisearch fb nikaziona picha zake na kuanza kuzifananisha na picha za yule mtoto wa rafiki yangu ki ukweli kama kuna ufanano fulani kati ya yule mtoto na yule kijana.
Sasa kila nikimpitia jamaa huwa namuangalia usoni natamani kumuambia ila sina kithibitisho ya yale niliyoambiwa na yule dada najikuta naumia mimi kwa sababu jamaa huwa ananieleza plan nzuri kuhusiana na familia yake haswa maendeleo ya kuwalinda watoto wasije fedheheka huko mbeleni.
Imefika muda nikimuona mke wa jamaa natamani nimpasukie ila ushahidi sina hebu wana mmu tushauriane. Je, hapa ni-mute au nitapike tu?