Nimetoka sasa hivi kupiga kura.
Kura ni siri lakini mimi nimepigia kura wagombea wa vyama vyote vitatu vikuu CHADEMA,CUF NA CCM,mpangilio nilivyotaja haufuati utaratibu wowote.
Pale kituoni watu wengi wa kata yetu nawafahamu kwamba ni CCM.Nikichanganya na mwenendo wa kampeni maeneo mengine nchini na kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao,dalili zote zinaonesha Jakaya Kikwete ndiye raisi anayemalizia awamu ya nne ya uongozi wa juu Tanzania.
Sasa natayarisha barua ya wazi kwa raisi huyu kutoka CCM.Nimeshaweka mezani vifaa vyote vya kuandikia isipokuwa maneno sijayapanga katika paragrafu zake.Kila nikijaribu nakuta sina maneno mengi na barua itakuwa fupi mno,haitopendeza.
Nawaomba wana JF tusaidiane vitu vya kujaza hii barua kwa Kikwete ili akiingia ikulu tu aikute barua yetu inamsubiri mezani kwake.