Nimepitia Bajeti ya 2022-2023 naona kuna kitu hakiko sawa

Nimepitia Bajeti ya 2022-2023 naona kuna kitu hakiko sawa

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Wana JF Naamini sote tu wazima.

Kwanza nianze na bajet ya mwaka jana.

Mwaka jana kulikuwa na stofahamu nyingi sana hasa baada ya bunge kuisha. Ilibidi kuongezwa kwa baadhi ya kodi ju kwa juu bila hata bunge kujua kama hiyo kodi ndio walikubariana ama la. Mfano ni Tozo za Miamala ya Simu, zilipanda hadi wabunge wakashangaa na tukaambiwa tuhamie Burundi. Na Mwisho wa Siku tukabidi tukope ili kuleta unafuu.

Pili, Mwaka huu naomba nianze na sehemu hii hapa. Makusanyo ya Mapato.

1655291291628.png


Ukiangalia hapo A (1 na 3). Kwenye maelezo tumepunguza sana tozo za ushuru wa forodha na VAT ila hapo kwenye jedwari makusanyo yanaongezeka toka Shs 1.4 Trillion mwaka 2022 hadi Shs 1.6 Trillion 2023 na Sh. 5.4 Trillion had Sh. 6.4 Trillion mtawalia kama ilivyo hapo juu. Sijui makusanyo yaningezwa na nini hasa kwenye huu mdororo wa uchumi duniani.

Ukiangalia hapo B (1). Michango ya Magawio ya Mashirika imeongezeka toka Sh 0.7 Trillion had Sh 2.57 Trillion. Na hatujaona uwekezaji wowote uliofanywa na Serikali wa kuongeza magawio kwa mara 3 zaidi.

Nitarudi kuendelea...
 
Back
Top Bottom