Nimepokea ujumbe kutoka Halotel kuwa nimejiunga na huduma ya AfyaCheck ambayo siijui na wala sijawahi kuisikia

Nimepokea ujumbe kutoka Halotel kuwa nimejiunga na huduma ya AfyaCheck ambayo siijui na wala sijawahi kuisikia

josephbnd

Member
Joined
Oct 7, 2023
Posts
8
Reaction score
6
Majira ya saa 10 jioni ya tarehe 09.12.2024 nimepokea ujumbe huu 1 na 2 (chini) kutoka mtandao wa Halotel Tanzania 🇹🇿 kuwa nimejiunga na huduma ya #AfyaCheck ambayo siijui na wala sijawahi kuisikia. Na mbaya zaidi wanasema huduma ile siku ya kwanza BURE baada ya hapo makato yanaanza ya 200Tshs kila siku. Kwa maana hiyo wanataka kunitumia meseji kama hiyo ya pili ili wakate salio langu. Naiomba mamlaka #TCRA ishushe ONYO kali dhidi ya huu wizi. Sitaki mimi.

1. [AFYACHAP]
Umefanikiwa kujiunga na huduma ya AfyaChap kutoka HALOTEL BURE kwa siku ya leo.
Utaendelea kufurahia huduma hii kila siku kwa gharama ya Tsh 200/Siku.
Tembelea AfyaChap Contents kupata dondoo mbalimbali na ushauri kuhusu Afya. Pia utafurahia huduma hii kwa njia ya ujumbe mfupi.

Kusitisha huduma tuma ONDOA kwenda 15513 au tembelea AfyaChap Contents.
Kwa maelezo zaidi tuma MSAADA kwenda 15513 au piga 100. Vigezo na masharti kuhusu huduma tembelea https://bit.


2. Wajawazito anzeni matumizi ya Folic mapema,
Vidonge vya Folic husaidia mtoto kutozaliwa na hitilafu mbalimbali kama Mgongo wazi,Ubongo wazi nk.
Screenshot_20241209_171033_Messages.jpg
 
Wapigie uwape onyo Kali wakutoe haraka.
 
Juzi walini ambia nimejiunga na HALO quiz , nimawapigia nikawaambia nitawashitaki TCRA wakanitoa chap na Hadi Sasa Heshima kidogo imeongekezeka,, hawajatuma Tena txts zao za ajabu
 
Back
Top Bottom