Nimepooza kiuno hadi chini, msaada tafadhali

Au ndio boch ameotaja mdau hapo chini
Hapana siyo BOCHI,ukiwa unatoka Kimara kuelekea mbezi kabla hujavuka traffic lights za Msuguli unaingia kushoto pana round about iliyoungana na barabara ya vumbi ya kuelekea BOCHI sasa wewe ingia na barabara ya lami inayoelekea kushoto kiasi cha metre 250 mbele kushoto kuna nyumba yenye floor mbili juu ina kigae cha grey ni hapo.
Au ndo Dr challe clinic
No anaitwa somebody Dr Kang
Mkuu madaktri nihao hao wakorea wawili mke na mume naje wanavipimo au
Ndiyo mkuu ni hao hao wawili kwa wagonjwa waliohudhuria muda mrefu waliniambia mwanzo kabla hawajajua Kiswahili waliweka wabongo kama wakalimani ila wakawa wanawaibia so wakaamua ku-stick kujua lugha kisha wakawafukuza so huduma wanazifanya wao tu.

Niwe mkweli,sijawahi kushuhudia wanatumia kipimo gani ila mgonjwa wangu aliingia chumba cha daktari alivyotoka akafanyiwa huduma za mwanzo wakati wa kulipa bill nikaomba mchanganuo wa hesabu so ktk kutajiwa kipimo kikawa Tsh 35,000/=,nilimuuliza mgonjwa wangu kama kweli alifanyiwa kipimo maana ilinishangaza kusema tatizo limeonekana akasema kweli alipimwa.
 
Hii si bochi ndo hospital peke iliyopo apo unapoelekeza ukiwa chini unaona matenk yake meusi
Mkuu nimetuma ufafanuzi hapo juu post #245 naomba ipitie unaweza ukaokota mawili matatu ya kukusaidia kama utakuwa interested kwenda au ukawa na swali lingine.
 
1.Tatizo limeanza lini?
2.Katika hosp ulizopita wanasema tatizo ni nini?
Nijibu hayo maswali mawili halafu nitapata pa kuanzia kukushauri
 
Mkuu nimetuma ufafanuzi hapo juu post #245 naomba ipitie unaweza ukaokota mawili matatu ya kukusaidia kama utakuwa interested kwenda au ukawa na swali lingine.
Mkuu nikweli kabisa nimefika mda huu mbezi kwa msuguli wanafanya kazi jumanne Hadi jumapili nanimke na mume maana nimefika nje ya geti nimekutana na mtu kaja clinic anaumwa mgongo kazuiliwa na mlinz kuwa leo hawafanyi kazi
 
Sawasawa,nilisahau kuliweka hili ktk maelezo yangu hapa mnisamehe sana.

Vipi lakini ulijaribu au ulifanikiwa kupata mawili matatu kutoka kwa huyu mgonjwa aliyezuiwa kuingia leo?shuhuda labda anaonaje huduma za hao watu?
 
Sikumuuliza nataka nirud asubuh
 
Sawasawa,nilisahau kuliweka hili ktk maelezo yangu hapa mnisamehe sana.

Vipi lakini ulijaribu au ulifanikiwa kupata mawili matatu kutoka kwa huyu mgonjwa aliyezuiwa kuingia leo?shuhuda labda anaonaje huduma za hao watu?
Hivi mkuu wanatibu nin na nin pale
 
Hivi mkuu wanatibu nin na nin pale
Binafsi nilimpeleka mdogo'angu alikuwa anasumbuliwa sana na kichwa,kupooza upande mmoja,kuna wakati mwili kuingia ubaridi na kusikia makelele kichwani kama vile mtu anapiga manyanga (hata leo alikuwa pale ameenda kupata matibabu),yote hayo amepona kasoro hilo la kelele kichwani ndo linamsumbua kwa sasa ila maumivu hasikii tena na hospital zetu hizi hayo maradhi hawakuyaona na vipimo vyote alifanyiwa tena kwa gharama kubwa na haviku-detect chochote.

Aliyenielekeza pale mkewe alipata stroke,alikuwa na matatizo ya moyo na maumivu makali kwenye mgongo,mbavu pamoja na magonjwa mbalimbali (kwa mujibu wake)ila baada ya kuhudhuria kwa hao jamaa miezi sita mfululizo mkewe shida zote zilionyesha kupungua kama siyo kuisha,siku zangu za mwanzo nikienda na dogo nilikuwa nauliza uliza kwa wagonjwa ninaowakuta pale ambao wengi walikuwa na maradhi ya viungo,stroke,moyo na mishipa so nahisi anatibu zaidi ya hayo pia vizuri ukienda kuuliza mwenyewe.

Wanatibu zaidi kwa sindano na dawa zao za asili na sindano wanachoma shingoni na kichwani pia mara chache kwenye makalio.
 
Pole Sana
Jaribu mbezi kwa msuguli kwa Dr Kang Kama alivoeleza mdau nimefika pale Leo nimekutana na wagonjwa wengi wamiguu na strock nahis wanatibu vizur maana nimekuta foleni ya watu
 
Pole sana mkuu : ebu jaribu hii imesaidia wengi tafuta asali mbichi og àlafu na mafuta ya zaitun unaanza kupakaa asali eneo lote lililoathirika unaacha unakaa nayo kwa muda kias kama saa moja hivi alafu unaoga unapakaa hayo mafuta ya mzaituni fanya hilo zoez kutwa mara 2 kwa muda mrefu utaona matokeo Mungu atakusaidia mkuu
 
  1. Tatizo lilianzaje?
  2. Kuna tatizo la mipango ya Mungu, na kuna tatizo linalosababishwa na wana nzengo
 
vipi wanatumia bima?
 
Samahani kwa kuulizia...je wanatumia bima
 
Siku ukimalizana na hizo tiba za hospitali na usione matokeo mazuri.Nitafute nitakutibu kwa mitishamba na baada ya mwezi utamshukuru Mungu kwa hatua utakayokuwa umeifikia.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…