Maleven
JF-Expert Member
- Sep 8, 2019
- 689
- 3,373
Yani kwa sasa mtu akisema anaenda kwenye nyumba ya ibada namuona kama “old school” mtu anaeishi maisha ya kusadikika,
Bado naamini kuna Mungu ila Mungu huyo hahitaji ibada wala hana habari na sisi, hakuna moto wala pepo.
Dini zote naona ni kama vikundi vinavyojinasibisha tu lakini hakuna ukweli na ni habari za kutunga.
Naamini katika kutenda mema na kushi na watu vizuri lakini siamini kama kuna adhabu au zawadi huko mbinguni,
Naona kua sisi ni kama wanyama na viumbe wengine, ukifa lako limeisha na hakuna habari inayoendelea.
Kwa upande fulan bado ninahofu na natamani imani yangu irudi, nimekua nikijikaza kushirikiana na wanajamii mambo ya dini ila ukweli nafsi haitaki.
Niko njia panda katika hili.