Nimepoteza kadi ya gari

Nimepoteza kadi ya gari

mbano

Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
46
Reaction score
21
Habari za leo wana Jamii.
Naomba msaada wako wa kunielewesha.
Gari langu lilipata ajali.kama unavojua ukipata ajali hapa Dar inakuwa dili kwa wenzetu vibaka.

Wakachukua kadi la gari.hati ya udereva na vitu vingine vingi tu.
Gari lilikuwa na hali mbaya sana ikabidi likatwe mbele na kunishauri ninunue upande wa mbele mwingine ili wafunge .na mie kweli nikafanya kama walivyonishauri mafundi.sikuwahi kuwaza kama itakuwa shida baadae.

Sasa shida inakuja Hapa nimefatilia TRA kuhusu kadi nimekwama kwenye chesis Number maana ile board walionibadilishia inasoma namba tofauti na zile za mwanzo za kwenye kadi.
Hivyo sijapewa kadi japo kuwa docs zote za manunuzi adi kuuingiza hapa na kuitoa Bandarini ninazo.

Waungwana naombeni Munisaidie nifanye nini mana nimechanganyikiwa mana nimeaambiwa hiyo ni kesi.
Na kama mujuavyo nchi hii kwa rushwa imekithili.

mama Janeth
 
Achana na kadi gari si unayo usihofu chapa mwendo muhimu kuwa na gari kadi nini karatasi tu.
 
mmh sijakoma mwenzangu ikifika wakati nikitaka kuliuza ntaliuzaje best wangu?
 
Habari za leo wana Jamii.
Naomba msaada wako wa kunielewesha.
Gari langu lilipata ajali.kama unavojua ukipata ajali hapa Dar inakuwa dili kwa wenzetu vibaka.

Wakachukua kadi la gari.hati ya udereva na vitu vingine vingi tu.
Gari lilikuwa na hali mbaya sana ikabidi likatwe mbele na kunishauri ninunue upande wa mbele mwingine ili wafunge .na mie kweli nikafanya kama walivyonishauri mafundi.sikuwahi kuwaza kama itakuwa shida baadae.

Sasa shida inakuja Hapa nimefatilia TRA kuhusu kadi nimekwama kwenye chesis Number maana ile board walionibadilishia inasoma namba tofauti na zile za mwanzo za kwenye kadi.
Hivyo sijapewa kadi japo kuwa docs zote za manunuzi adi kuuingiza hapa na kuitoa Bandarini ninazo.

Waungwana naombeni Munisaidie nifanye nini mana nimechanganyikiwa mana nimeaambiwa hiyo ni kesi.
Na kama mujuavyo nchi hii kwa rushwa imekithili.

mama Janeth

Ni karatasi gari si unayo? Kweli JF Kiboko

Nenda kwa mamlaka(TRA) inayohusika watakupatia kadi ingine baada ya kupitia hatua kadha kama polisi ripoti n.k
ingawa ww ulikuwa mzembe ulikuweje na kadi orignal ndani ya gari? ndio ulikua umetoka inunua?
 
Kwa uzembe kweli najutia.ndo nilikuwa nimetoka kununua ndugu yangu.
 
Wewe mama janet,nenda tra kitengo wanakoprint card wakiamua kukusaidia wanaweza kukuuliza copy ya kitambulisho na watakuprintia card nyingine
 
Kwanza pole. Fanya kama ifuatavyo:
(a) Tafuta copy ya kadi ya gari yako ambayo umepoteza.
(b) Nenda kituo cha Polisi waambie wewe umepoteza gari ya gari, watahitaji hiyo photocopy ili waridhike kuwa wewe ndio mwenye gari. Usijali kwa sasa hivi kama umekata kipande na kuweka kingine. Achana na mambo ya chasis no. nk. Waombe wakupe 'Police Lost report.'
(c) Wakisha kupa hiyo 'police Lost report', nenda nayo TRA sehemu wanayo andikisha magari, waoneshe hiyo 'Police Lost report', watakuambia uende benki ukalipe sh. 10,000.00 kisha mwandikie barua meneja wa TRA kuomba 'duplicate copy' ukiambatisha vifuatavyo: 1. 'Police Lost report'

2.Bank payment receipt ya sh. 10,000.00

3. Kitambulisho ( photocopy) ( cha mpiga kura kinatosha)

(d) TRA watakupa kadi nyingine baada ya siku thelathini (30 days)

Kila la heri
 
Back
Top Bottom