Mzunguko wa mwanamke huwa unatawaliwa na hormones ambazo kiasi chake kwenye damu kinatofauti kufuatana na siku za mzunguko, na hivyo mwili unarespond tofauti. Si kitu cha ajabu matiti kujaa na/au kuuma kidogo ukikaribia hedhi!
Kuna dawa za uzazi wa mpango ukitumia unakuwa hupati hedhi (sindano ya Depo-Provera) kwa angalau miezi mi3, ndiyo ulikuwa unatumia? Ila ukiacha baada ya miezi mi3 hivi unaendelea kupata hedhi.
Umri wa miaka 40 unaanza 'menopause' ambapo mwanamke anakoma kupata siku zake. Mara nyingi huwa haikomi ghafla, kunakuwa na mabadiliko ya mwezi mara unapata mara unakosa, baada ya muda hedhi inakoma kabisa...ni kawaida (soma kuhusu menopause au kukoma hedhi).
Daktari uliyemuona kama ni wa magonjwa ya wanawake alikuwa anatosha kukupa maelezo kuhusu menopause na uzazi wa mpango. Unaweza ukawa na vivimbe yes, lakini mara nyingi vivimbe (fibroids) huongeza damu kutoka wakati wa hedhi, na sio kukausha (except labda ukiwa umeshakoma hedhi). Tafuta daktari wa magonjwa ya wanawake kwa uchunguzi na ushauri zaidi.