Nimeridhika kabisa: Mbwana Samatta hakuwa msaada kwa Aston Villa, Watkins ameonesha utofauti mkubwa

Ndo mana huwa nilitamani sana bahati aliopata samatta angepata msuva angekua zaidi ya pale alipo samatta sasa hivi!!!

Msuva ni fighter hata uchezaji wake katika timu ya taifa mnauona kuliko huyo samatta!
 
Itakuwa huna au uwezo wako wa kuelewa Mambo ni mdogo.pole

Yupo njiani sasa anarudi kuja kulitetea Taifa lake kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi. Lazima mkubali kumpa heshima yake.

Haiwezekani kijana amepambana mpaka hapo alipofikia, halafu nyinyi kutwa kumpiga tu majungu.
 
sawa MCHAWI...endelea kumuwangia pia akiwa huko uturuki mana ndio kazi uliyonayo
 
.[emoji23][emoji23][emoji23] kila wiki yuko mahakamani
 
Wewe unapata sh ngapi kwa week?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
utamaliza nguvu zako tu mkuu kwa raia wa aina hio ...mambo ya uchaguz pia yanatuchanganya
 
Sisi Wahaya tunasema, "Ekyawe kijunda nokara"! Mimi nitaendelea kumuona Samatta ni kiboko sio zaidi ya Watkins tu bali zaidi ya Messi na Ronaldo!
 
Yupo njiani sasa anarudi kuja kulitetea Taifa lake kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi. Lazima mkubali kumpa heshima yake.

Haiwezekani kijana amepambana mpaka hapo alipofikia, halafu nyinyi kutwa kumpiga tu majungu.
Mtoa mada kaongelea uwezo wake kuwa Epl sio kutetea taifa, tatizo huwezi kuchanganua Mambo. Kwani kujitetea Taifa Kamzidi Ngasa, Canavaro, Msuva au Juma kaseja?? Tena kea taarifa yako msaada wake n mdogo Sana kwenye timu ya Taifa kuliko kina Msuva
 
kwamba samatta ni utopolo..dah umasikini mbaya sana
Ni utopolo kwa huyo anayefananishwa naye lakini kwa wachezaji wa TZ Samatta ni Torres wao, punguza mahaba usijekufa kabla ya siku zako maana imeandikwa kila kitu tuwe nacho kwa kiasi.
 
Mtoa mada kaongelea uwezo wake kuwa Epl sio kutetea taifa, tatizo huwezi kuchanganua Mambo. Kwani kujitetea Taifa Kamzidi Ngasa, Canavaro, Msuva au Juma kaseja?? Tena kea taarifa yako msaada wake n mdogo Sana kwenye timu ya Taifa kuliko kina Msuva

Huu mjadala tuufunge. Naona unanichosha tu. Nisije nikawa nabishana na mke wa mtoa mada humu! maana jina lako halijafungamana na jinsia yoyote ile na kwa namna unavyonitolea maneno ya dharau na maudhi, inanipa walakini.
 
Wewe unapata sh ngapi kwa week?

Laki mbili na nusu! Nina digrii huku Samatta akiwa kaishia kidato cha nne tu! Ndiyo sababu namheshimu na kuwapuuza wale wote wanao mchukulia kama mtu wa kawaida katika kipengele chochote kile, akiwemo huyo Mrs Petro hapo juu.
 
Nyinyi watu wengine sijui mpira huwa mnautizama vipi!? Hebu leta takwimu sammata alipoteza clear chances ngapi, alianza game ngapi alifunga ngapi, hapo nfio tutaweza kujadili..

Ni kwamba katika game takriban kadhaa zilizochezwa villa hii sio villa ile. Tizama takwimu za aston villa hii na aston villa aliyoikuta samatta.

Unaposema samatta kimeenda kimerudi, samatta mwenyewe aliikuta timu dhofulhali, kaenda pale dirisha dogo kaikita villa ipo hovyo kama alivyoiacha.
 
Hamna kitu mle,hata kwenye reserve hawezi kupata nafasi
 
Naomba pia utuambie Watkins katengenezewa nafasi ngapi na Samatta alitengenezewa ngapi ili tuwianishe. Mnaoichambua Aston Villa baada ya Samatta sijui ni kwa nini huwa hamtaji mabadiliko mengine yaliyofanywa na timu. Asiyefuatilia mpira anaweza dhani kuwa Aston Villa wamemsajili Watkins pekee.

Pia asiyejua mpira anaweza kudhani kuwa Aston Villa bado wanacheza na mfumo wao uliowagharimu msimu uliopita wa 3-4-3. Ambapo walau nusu ya kwanza ya msimu uliopita walikuwa wakishambulia bali kuanzia Januari ya Samatta hawakuwa tena na attacking threat kwa wapinzani. Sababu mojawapo ikiwa kushuka kiwango na uchoyo wa mchezeshaji wao bwana Grealish.

Napenda wachambuzi wa sakata la Samatta Aston Villa wawe wanakuja uchambuzi uliokamilika.
 
Ingekuwa vizuri kama ungeanza na kiwango chako uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…