Nimerikoroga

chimala

Senior Member
Joined
Jul 2, 2010
Posts
162
Reaction score
34
Baada ya kukaa mda mrefu bila kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi,nimejikuta naangukia penzi la kaka mmoja tuliyefahamiana miaka mitatu iliyopita, huyu kaka aliniambia kwamba ananipenda toka mwanzo tuliponana, nikampotezea ,hakukata tamaa amekuwa akinisumbua sana kwa simu, sms, email mpka nilipoamua kumkubalia mwishoni mwa mwezi wa pili. Toka tulivyokubaliana kuanzisha urafiki, mawasiliano akawa hataki i tena, yaani atapiga simu siku anayotaka kuonana na mimi tu, hilo lilinikera sna nikaamua kuwa nampigia mimi,mesage nikituma hajibu, baada ya week mbili kupita nikiwa nikipiga simu hapokei kabisa nikamtumia mesage ya kumbembeleza sana kwa nini hapokei simu akasema kwamba mda mwingi huwa anakuwa hana simu, anaweza kuwa ameichana kwenye gari,au kaisahau nyumbani,

Baada ya kuniambia hivyo nikaamua kuwa nampigia na line nyingine tofauti cha ajabu akawa anapokea mda wowote ntakao piga, sema nikawa siongei nakata simu,
nikagundua kuwa hataki tu kupokea simu zangu, kitu kingine nilichofanya nikajoin facebook kwa username nyingine, nikamtumia request na message kwamba nimependa relationship status yake kwani aliandika yupo single na ningependa kuwa girlfriend wake. Lol jinsi alivyorepond sikutarajia kwanza alikubali kuwa mi ntakuwa mpenzi wake na mungu akijaalia ntakuwa mke wake, tulivyokuwa tunaendelea kuchat nikamuuliza una mchumba ama girlfriend akasema yeye yupo single na nisiwe na shaka kabisa, akaniomba number ya simu ili anitafute akitoka kazini, nikapiga chenga chenga sikumpa number siku ya kwanza, siku ya pili nikakuta message nyingi sana zikinisihi nimpe number ya simu kwani ana hamu sana ya kuongea na mimi, ndipo nilipoamua kumwandikia number yangu,sasa tangu nimempa number yangu hajatuma ujumbe tena facebook na mimi sijawasiliana nae week ya pili hii.

Wanajamii hivi huyu kijana ananipenda au nichape lapa tu kabla sijainvest mapenzi mazito kwake, kuumizwa na mapenzi tena sipo tayari
 
Hujalikoroga bibie huo ndo ujanja wa kutambua ukweli. Hapa sioni kama unaomba ushauri gani maana ushamjua jamaa sio kabisa.

Piga mbio kama za marathoni
 
Kimbia kama kibaka...yani hata usiangalie nyuma.Inawezekana anakuadhibu kwa kumzingua mwanzo sasa kaona akugeuzie kibao.
 

Hongera kwa kujitahidi kuvumilia....(hebu naomba ufafanue hizi posts)

Pia naomba kupata ufafanuzi wa hii post yako ya January, kabla sijachangia


Sasa hivi naogopa hata kuchangia..utunzi umekuwa mwingi sana!!

Sasa sijui nichukue lipi niache lipi??
 
Kimbia kama kibaka...yani hata usiangalie nyuma.Inawezekana anakuadhibu kwa kumzingua mwanzo sasa kaona akugeuzie kibao.

Ngumu kweli kujua mwenye upendo wa kweli
 

Ameona hulipi au huna mvuto au umechuja au hujitumi kunako

Soma alama za nyakati using'ang'anize usipo pendwa we chapa lapa usipoteze mda wako.
 
Alipokuwa anakutafuta simu ilikuwa on masaa yote sasa amepata alichokuwa anataka
anajidai simu amesahau hapa mara pale tabia umeiona
hakuna mapenzi kabisa hapo kimbia na usigeuke nyuma
usitume msg yoyote kaa mbali kama mbingu na ardhi
 



Huyu tulishaachana, hiyo January alitaka kuja kunitembelea nikampiga marufuku asije, na mawasiliano nae tena sitaki
huyu ,mpya nimeanza nae mwezi wa pili mwishoni sijui kama ulisoma vizuri hizo post
 

hahahhahhaahaha hoo my mbavuz.
JF kwa kuchokonoa nawaaminia

jamani kumbukeni kuwa consistent mnaaibika mnajiona haa!!lol
 

Asante sana mkubwa tusaidiane kujenga nchi
 
Changanya karata zako vizuri na angalia moyo wako unasema vipi na uamue kulingana na moyo wako,pia yafaa umuweke wazi ajue ukweli na natumai itamsaidia hapo baadae kuwa na msimamo wa kutulia na mpenzi mmoja kama utaamua kuachana nae.
 
Huyu tulishaachana, hiyo January alitaka kuja kunitembelea nikampiga marufuku asije, na mawasiliano nae tena sitaki
huyu ,mpya nimeanza nae mwezi wa pili mwishoni sijui kama ulisoma vizuri hizo post

Ulipost July 2010 kwamba mpenzi alitaka muwe marafiki wa kawaida

then ukapost Jan 2011 kwamba unaomba ushauri mpenzi wako anataka muwe good friend..

Hao ni watu wawili tofauti au ni yule yule??

Kama huyu wa sasa ni kweli amefanya hivi...na amekuonesha dalili zote toka mwanzoni, kwa nini ulihangaika kumfuatilia kwenye mitindao (wivu wa hali ya juu)..ulipaswa kumpotezea muda mrefu tu.. au kwa sababu ana gari??

Ila umenichanganya kusema kweli..
 
Mpendwa soma uelewe post, sio unakurupuka tu hapa, zisome hizo post utaelewa mpenzi alienianmbia kuwa tuwe gud friends ndo alitaka kuja kunitembelea
 

Hakuna utetezi hapo kachemsha ni wale wale kina shigongo type comedy nyingi sana humu siku hizi
 
Reactions: Mbu

hahahahahahaha!!
Mpendwa unatumia kinywaji gani vile?
 
Maswali mengine bana.....
Ukiona manyoya si ndo keshaliwa?
 
Reactions: Mbu

Pole kwa kuchanganyikiwa, ni mtu yule yule aliyetaka tuwe gud friends ndo akataka kuja kunitembelea nyumbani, huyu ninaemsema hapa ni mpyaa tumeanza urafiki mwishoni mwa february
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…