Mkuu ili nipate leseni ya management consultancy natakiwa niwe na vitu gani?
Bahati mbaya sijawahi jiuliza kitu hicho kwa hapa tz, pili Managent ni pana sana bora unge specify
Kama HR Managent , Service Managent, IT Managent, Operation/production Managent, Strategic Managent, Marketing Managent na nyingine nyingi.
Nachojua kwa taaluma yeyote ili uwe consultant lazima uwe na knowledge ya hilo eneo husika at least Bachelor degree plus experience at least 5 years na kama hapa nchini ipo professional Board ya hiyo taaluma wakutambue/ yaani uwe registed as professional consultancy kama ilivyo NBAA, PSPTB, ERB, CRB n.k
Bahati mbaya Tz hatujawahi kuwa Professional Management Board na km ipo sijawahi isikia
Nashauri kama ni ajira yako bora kuchukua leseni ya kawaida tu ya General Business Consultancy ambayo hutolewa kila wilaya watakuomba vyeti vyako vya degree ya business mfano BBA tu, fee ni sh 200,000= au 300,000=