Nimesema Sipendi Ujinga

Nimesema Sipendi Ujinga

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,274
Reaction score
6,595
Wabongo bhana yani kila kitu kinacho tokea lazima watakataftia KAMSEMO

mfano yalivyo letwa mabasi ya mwendo kasi , kaliletwa KAMSEMO mwendo kasi , ikawa kila kitu ni mwendo kasi , tuliona nywele za mwendo kasi , tai, simu, glass, suti, nk KAMSEMO hako ka mwendo kasi kalizimwa

ikaja kupatwa kwa jua, ikawa kila kitu ni kupatwa hadi majina yaliletwa mfana mwakupatwa , nk KAMSEMO hako bado kapo ila kwa mbaali

Kakaletwa KAMSEMO kapya "Mungu anakuona /anawaona/anatuona" kamepotelea wapi sijui

likaja tukio la tetemeko la aridhi huko bukoba , duh ikawa kila kitu ni tetemeko hadi tetemeko la ndoa , nk

sasa wabongo wamekuja na nyingine hii inaitwa "SIPENDAGI UJINGA /HATUPENDAGI UJINGA" haka KAMSEMO sasa ndio habari ya social media , yani kila meseji mwishoni usipokuta hako KAMSEMO meseji hiyo haijanoga kabisa , sasa na mimi namalizia kwa kumchana anae leta hivi vimsemo , na mmwambie nimemchana laivu

Sipendagi ujinga mimi
 
Aise hata mimi nakuchana ewe mleta mada . Sipendagi ujinga kabisa.
 
Mimi mwenyewe sipendagi ujinga wa kupost ujinga kama huu wako(in a polite lang.)
 
Back
Top Bottom