Kwa kweli hali tunavyofikirishwa na majilabu ya Chama tawala kuwa wataiboresha Tanzania kuwa ya aina yake! Nashangaa sana tunaaminishwa tupo kimaendelea tupo uchumi wa kati na jana juzi tunaanza kuaminishwa kuendea uchumi nambari moja, nikazidi kushangaa na kuwachwa kwenye mataa.
Nina wasi na uchumi huu unaotajwatajwa na tunaoaminishwa kama unatuhusu sisi wanyonge, nimeona ile kauli ya Mnyonge myongeni lakini mpeni haki yake umegeuka na kuwa mnyonge msimnyonge lakini musimpe haki yake.
Rais Suluhu kuingia tu ameingia na gear ya kupandia mlima na ya kushukia mlima baada ya mkaguzi kuweza kupumua na Rais nae kupata pa kuchungulia au pa kuanzia kwa kusema anahitaji ukaguzi wa mahesabu kuanzia January na pia kuwasimamisha kazi wakuu wa bandari, Tunaweza sema yajayo yanafurahisha?
Mashaka ni kuwa sasa Rais ametafuta Mpango, kwa kuwa ni mapema huwezi juwa ni mpango gani? Ni wa yuleyule aliyeondoka na sasa mpango umepandishwa grade na ahadi ni za kufuata nyayo. Mitandaoni kwa wananchi wenye uchumi unaowaruhusu kuingia huko malalamiko yameanza kuwa raisi ameokota bokorewa au lulu?