Nimeshangaa kukuta bei tofauti za mafuta ya Petroli katika Petrol Stations mkoani Kagera

Mgodo visa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Posts
3,590
Reaction score
3,632
Kama kichwa cha habari kilivyo hapo juu...

Nimeshangaa kukuta bei tofauti za mafuta ya Petroli katika Petrol Stations mkoani Kagera.

Hivi hawa Ewura ambao ndio wadhibiti wa Nishati hii (Petrol) katika kusimamia Ubora ikiwa ni pamoja na usimamizi wa Bei,
mbona huku vituo kila mmoja na bei yake..!!

Je lile azimio la kila Mkoa kuwa na bei elekezi linaishia huko Mikoani..!

Swali je Mafuta ya huku Kagera yanatoka wapi, labda pengine ni nchi jirani Uganda hivyo mnapoteza haki ya Udhibiti wa Ubora pamoja na Bei.

Tunaomba mamlaka ziingilie kati, ili wananchi tupate kile tunacho stahili..
 
Mkuu, ebu weka hapa hizo bei mnazo uziwa mafuta huko Kagera, ili tulinganishe na bei elekezi...
 
Weka bei tuone . kumbuka bei ya mafuta kagera huwa juu
 
Tatizo huku ni kila mmoja na bei yake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…