poleni sana. hiyo inajulikana kama juvenile diabetes type 1. inaweza kusababishwa na vitu viwili:
1.Autoimmune- ndio sababu kuu, virusi vinastua mwili kutengeneza sumu ya kinga, ambayo mwisho zinaharibu betta cells ambazo ziko kwenye pancreas na kusababisha insulin isitengenezwe kwa usahihi. inashukiwa kuwa ni Coxsackie B4 virus ama Cytomegalovirus
2.mara chache inatokea shambulizi makali kwenye pancrease (sijui ndo yaitwa kongosho?),ama kwa sababu zozote za kiugonjwa pancrease kuondolewa kwa operesheni
kuna uwezekano wa kuipata kwa 6/100 endapo ndugu yako wa tumbo moja anayo( so ni muhimu kuwaangalia kwa ukaribu hao nduguze manake type 1 diabetes ina-attack ghafla sana hivyo ni hatari). Akizingatia ushauri wa wataalamu haina madhara makubwa sana na atakua salama,inshaallah.