Nimeshangaa kuona mtoto wa miaka 2.5 anaumwa kisukari.

hakuna ugonjwa wa kurithi hizo ndio imani potofu sasa, mie nakueleza hilo ni pepo huelewi, na katika watu wanaosumbuliwa na mapepo ni hao wanaojíita watumishi wa mungu, kwahiyo waeleze hilo sio tatizo la kihospital hiyo spiritual problem waombe mtoto atapona kwakifupi wazazi wa huyo mtoto ndio imani zao zinaumwa ndo maana wamekubali mtoto wa 2.5 anasukari hiyo ni maajabu hata kwa madokta
 
Unajuwa mi kuanza kudhani mtoto wa miaka 2.5 anaweza kupatwa na mapepo mpaka kisukari ni jambo lisiloniingia akilini. mapepo yaende kwa mtoto kufanya nini?. king'asti alikuambia vizuri kuwa hiyo inaitwa juvenile diabete, nikakuambia maji ni uhai. umeisoma vizuri ile blog ya maji? (maajabuyamaji2.artisteer.net).

kwa kawaida siku utakapozidiwa utakimbizwa na ambulance ICU, njiani utatundikiwa dripu la maji/chumvi. Utangulizi | maajabu ya maji
 
kiongozi sio kwamba ushauri wako nimeutupa.ila ninajaribu kukusanya ushauri then nipate pa kuanzia.
 
mkuu afadhari umerudi, leo tu nilikuwa nalijadili jambo hili na mtu fulani, ningependa kujuwa iwapo mtoto huyo mlikuwa mnampa soda au juisi zingine za viwandani? tafadhari nitafurahi ukinijibu na mimi nitakujibu tena
 
ki-ukweli soda alikuwa anakunywa ila mala moja moja saaana yaani sikukuu mpaka sikukuu.
 
ki-ukweli soda alikuwa anakunywa ila mala moja moja saaana yaani sikukuu mpaka sikukuu.

hapa nipo geita nalala kesho nitakuwa mwanza tena kwa mgonja. Nitasoma maendeleo yake kisha nitayaweka hapa.
 
Ahsante sana Dr umefanya vitu vyako hapa. Bandiko hili limeenda shule sana.
 
hapa nipo geita nalala kesho nitakuwa mwanza tena kwa mgonja. Nitasoma maendeleo yake kisha nitayaweka hapa.

tarehe 13 sukari ilikua 30.5 leo sukari kwa kipimo cha asubuhi saa nne ilikuwa tano.leo mchana sukari ipo 20. Bado jioni sijui itakuwa ngapi.kifupi haileweki inapanda na kushuka.kuhusu uzito wa mtoto ana kilo 13.
 
upo geita sehem gani ndugu?

nime kwisha toka geita.hivi sasa nipo mwanza.ila kesho tena nitakuwa geita mitaa ya twiga.au katundu kaswela.
 
tarehe 13 sukari ilikua 30.5 leo sukari kwa kipimo cha asubuhi saa nne ilikuwa tano.leo mchana sukari ipo 20. Bado jioni sijui itakuwa ngapi.kifupi haileweki inapanda na kushuka.kuhusu uzito wa mtoto ana kilo 13.

Ni lazima kumfundisha yeye, wazazi wake na hata hausi geli nidhamu ya kudhibiti anachokula (diet control). Kila chakula kina kiwango fulani ya glukosi, naambiwa labda ni mchicha tu usiokuwa nayo, nikiwa mgonjwa wa kisukari pia (IDDM) namshauri yafuatayo:
1. Apunguze matumizi ya wanga -- haikwepeki bali kiasi kipungue. Asiwe anakula milo mikubwa -- kidogokidogo lakini kwa frequency zaidi.
2. Asahau kuhusu soda na juisi za viwandani, anywe maji zaidi. Juisi natural ni nzuri ila sio kwa matunda yote, k.m. maembe yana kiwango kikubwa zaidi cha sukari hivyo yaepuke.
3. Kama amesha anza kutumia dawa k.v. insulin au vidonge basi muhakikishe kuwa dozi inafuatwa bila kukosa.
4. Magonjwa k.v. homa, mafua n.k. yanaweza kusababisha kuongezeka au kupungua kwa kiwango cha sukari, kuweni makini

NB: Vipimo vichukuliwe asubuhi kabla ya b/fast, mchana kabla ya mlo na jioni pia kabla ya mlo. Vipimo vya baada ya mlo mara zote (au mara nyingi) vitasoma namba kubwa tu.

Nitakuja tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…