Nimeshangazwa na kukuta mabati yamepanda bei

Bati ya migongo midogo ya futi 10 upana wa bati cm 90 (migongo 12)....kampuni Sunshare
Bati la msauzi hiyo bei naweza kuamini..Mshikaji wangu kanunia G30 Bati upan 90cm futi 10 kwa 34k. Kwa sasa siwezi bisha. Zile za versatile zilikuwa 37k mwaka jana.
 
Huna akili, negative maana kwamba mtu akienda kuweka mafuta analipwa ama? I hate kujenga hoja na dumb ass kids...

Niambie unachokijua
Utajua hakuna unachojua, kipindi cha corona bei ya msfuta ghagi ilifikia-negaitve!

Shida ilikuwa ni kusimamisha uzalishaji wa mafuta ni gharama zaidi na wakati huo huo visima ( tank) vya kuhifadhia mafuta ghafi vilikuwa vimejaa"

Huko duniani ilibidi wapunguze stock kwa kulipia kiasi cha pesa!

Wakati huo sisi tuliuziwa mafuta 1600@lt.!
 
66
 
Wapi huko mkuu,Tanzania hii au Ni Burundi? Bati gauge 30 limepanda kutoka 18,000/= Hadi 22-25,000/=, hii Bei yako ya 41,000/= kwa gauge 30 imeanza lini?
Usibishe, nenda sokoni.

Mwezi mmoja nyumba viwandani Kama bati bomba, tantu, snowbati ziliuzwa 23,000 gage30 saivi zinauzwa 29,000 kiwandani, je mtaani Bei gani?

Bati 28gage, nyeupe simba dumu mtaani Dar inauzwa wastani wa 35,000 kwa pisi.

Na viwanda vyote vina uhaba wa bati wengine wamefunga kwanza.
 
Sababu zimeshaelezwa ni inflation ya Dunia tunakoagiza raw materials na kupanda Kwa shipping costs, sababu zote ni out of our control.
 
Bongo bei ya mchongo! Ifikie mahali mafuta yangeondolewa charges zote ukiachilia tu kodi!

Yale makorokoro mengine yafidiwe na Tozo😎 maana tozo imekaa kijanja janja sana serikali inatengeneza hela nyingi mno kupitia Tozo hizi ambazo hawataki hata kutoa report ya makusanyo yake.
 
Ukirudi next week bati utazikuta 50 [emoji3]
Maisha ya ujenzi hivi sasa hayaelezeki. Nondo mm12 inakaribia 30,000/= Kitila Mkumbo yupo yupo tu. Maisha magumu sana. Wauzaji wenyewe wanalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…