Nimeshangazwa na Matokeo ya Kidato cha Nne 2021

Nani anakumbuka kipindi cha " BIG RESULTS NOW" 😁😁😁
 
Acha wivu bwashee
 
Ambacho mnasahau ni kwamba form four kufikia 2025 itatambulika kama elimu ya msingi na sio sekondari tena,

kingine nikwamba kuna kitu kinaitwa C.A, kwenye matokeo ya mwaka huu kimepewa kipaombele sana haswa kupunguza dv zero kwenye shule za kata!!

So kwa namna moja au nyingine. Standardazation imefanyika [emoji123]
 
Division 1 zimekuwa nyingi, hasa ukizingatia kuwa siku hizi 75% ni A. Lakini pia penalt za somo la Hisabati hakuna tena.

Yumkini, ndio maana hata somo la Hisabati limefanya vibaya mno maana hakuna penalt tena.

SUKAH
 
Hawa Necta sijawahi kuwaelewa tangu wanibandikie div 2 O' level na kunibandikia masomo yote C.

Nilikuwa na uhakika masomo kama chemistry, Biology,History na Geography ningepata A kama ni kufeli sana isongeshuka B ila nikabandikiwa C.

Hadi leo naamini huwa wana sahihisha kwa umakini shule walizokariri kuwa wanafanya vizuri.
Ndio maana utasikia St Francis, Kemebos kila mwaka
 
Mfano Mkubwa Ni Mdogo wangu Ambaye Amefaulu kwa Division 1 ya 7 huku nikijua Fika Kichwa chake ni Kigumu, na Hajawahi Kuwa Kwenye 20 bora Darasani Kwao. Inanipa Wasiwasi Kwa Form 6
Hii chai... Ufaulu huo wa kidato cha ngapi!??!?
 
Markers wenyewe wanaenda kwa kujuana, unafikiri kuna kitu hapo ni kuangalia na siasa zao tu
 
Wakati wa mwendazake sijui kama uliweza kuhoji namna hii. Sijui kama uliwahi kushangazwa na NECTA hii hii iliyokuwepo enzi za mwendazake na matokeo waliyokuwa wakitoa
 
Mkuu umeongea jambo zuri sana. Tatizo ni mitihani ya kubet inayowapeleka wanafunzi shule za sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika. Tazama video ifuatayo kwa ushahidi zaidi; sipendi kuongea maneno matupu. Tazama video πŸ‘‡
Your browser is not able to display this video.



Na huko sekondari mitihani ya NECTA imerahishishwa kwa makusudi ili kuwafaulisha wanafunzi kisiasa. Tazama mtihani wa Biology wa NECTA 1999 ulinganishe na mtihani wa NECTA 2017 utapata jibu mwenyewe. Zamani kupata divisheni wani halikuwa jambo la mchezo. Maswali rahisi kama haya (2017) hata mkulima ambaye hakwenda shule atapata divisheni wani misa ya kwanza tu!

NECTA 1997

NECTA 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…