Nimeshangazwa na Matokeo ya Kidato cha Nne 2021

Ila tuache utani jamani
Shule za Serikali wanafunzi wanajitafutia maarifa mtaani
Si ajabu kukuta mtu kapata B Geo ila akikwambia alivyohaso utamuonea huruma.
 
He! Hakuna penalt ya hesabu?
 

[emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2299][emoji2379][emoji2379][emoji2379][emoji2379][emoji2379]

Hii ni Kali Aiseee.
 
He! Hakuna penalt ya hesabu?

Duh, hiki kitu kumbe wengi hawajui ee…?
Penalt zilishakufa miaka mingi sana iliyopita…
Hawa nilioonyesha miaka ya nyuma wangekuwa na three..lakini wana F za hesabu na wana division 1 na 2.
 
Hivi hamuelewi kuwa kwa sasa kidato cha nne ndiyo shule ya msingi?nina uhakika mtoto akifika kidato cha nne atakuwa anajua mambo ya msingi....siasa ipo
Unaongelea mtaala gani mkuu? Mi nimeshika kitabu Cha mtoto wangu wa Darasa la tano naona wanasoma vitu ambavyo Enzi zetu tulisoma O level. Nimeona wanasoma Hadi Reproduction
 
Duh, hiki kitu kumbe wengi hawajui ee…?
Penalt zilishakufa miaka mingi sana iliyopita…
Hawa nilioonyesha miaka ya nyuma wangekuwa na three..lakini wana F za hesabu na wana division 1 na 2.
View attachment 2084581

Hapa ndio Maana tuna Mashaka na Division 1 unakuwaje una Division 1 na Basic Mathematics una ‘F’ huyu akienda Kusoma PCB au CBG akakutana na Na Mathematics Hawezi kutoboa au ile ya Advance wameifanyaje? Kwenye baadhi ya Combinations?
 
Real eyes realize real lies..

We have been conned big time
 
Duh, hiki kitu kumbe wengi hawajui ee…?
Penalt zilishakufa miaka mingi sana iliyopita…
Hawa nilioonyesha miaka ya nyuma wangekuwa na three..lakini wana F za hesabu na wana division 1 na 2.
View attachment 2084581
Kumbe serikali imeondoa penalty kwa makusudi ili kuongeza idadi ya divisheni ones kisiasa 😳 Mungu anawaona kwa kweli; ndio maana nchi hii imelaaniwa!!!! 😳 😳 😳
 
Duuh unajua hii kitu huwa natafakari sana jibu nakosa .
Kuna watu walikuwa na points 26. Kuna watu walikuwa na points 33-35.
Cha kushangaza matokeo yaliporudiwa
Wale wenye 33,34,35 wakaenda mpaka points 21 nk. Huku wengine wenye 26 wakabakia vilevile
 
Kama wamekosida CA kweli hawako serious...yani CA ambazo walimu wamejaza bila hata kuwa na hizo test amabazo zilitakiwa kujazwa.

Kwa mfano mwaka huu wameondoa project kwenye CA wakaweka mock.cha ajabu kuna wanafunzi walijaziwa matokeo ya mock wakati hata hawakufanya.mfumo haruhusu uache wazi hata kama mwanafunzi hakufanya mtihani
 
Mi pia ni muhanga wa 2012, kuna shida saba NECTA.
 
Kuna siasa nyingi sana mkuu.

Wakati mwingine wanafanya standardization kuaminisha umma elimu iko juu,sababu mwananchi wa kawaida anachojua kupata hizo one na two nyingi badi elimu ni bora. Siasa ni nyingi Sana kwenye matokeo ili kupunguza au kuondoa kelele.

Kidato cha pili ndiyo usiseme. Naongea haya kwa uzoefu wangu.
 
Bado sijapata matokeo ya kidato cha nne 2001. Naomba msaada wa namna ya kuyapata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…