EEM M
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 459
- 937
Wasalaam Watanzania!
Natumaini wote ni wazima wa afya kabisa na tunaendelea na kujilinda.
Kwanza kabisa naomba ku-declare interest, Mimi sio Mwanachama wa chama chochote cha siasa na wala sijawahi kugombea nafasi yoyote ile katika chama chochote cha siasa bali ni muumini wa HAKI na Viongozi wazuri bila kujali itikadi za vyama vyao.
Pili nitoe Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliowapoteza wapendwa wao kwa kutekwa, kuuliwa au kupotea/kupotezwa na naamini damu zao hazitoenda bure Mungu atawalipia hapa hapa duniani.
Niende moja kwa moja kwenye mada!
Wiki kadhaa zilizopita Bungeni kuliibuka hoja ya dharula ili kujadili kukithiri kwa vitendo vya watu kutekwa na kupotezwa lakini Bunge chini ya Spika Tulia Akson lilikataa kujadili hoja hiyo huku akisema wabunge waache kutumia hisia huku akitolea mfano baadhi ya matukio ambayo watu walijiteka na wengine waliuliwa na waganga wa kienyeji katika kutekeleza imani za kishirikina.
Katika matukio mengi ya kutekwa na kupotezwa wahanga wengi wamekuwa ni wale wenye mlengo wa CHADEMA, wanaharakati na ambao mara nyingi wamekuwa wakiikosoa serikali hasa watumiaji wa mtandao wa X.
Hoja hiyo iliibuka Bungeni kwa siku mbili mfululizo huku Spika tulia akiipiga chini na kukataa Bunge lake lisiijadili kwa siku zote mbili.
Licha ya kwamba TLS ilitoa orodha ya Majina zaidi ya 80 ya watu waliopotea/kupotezwa, kutekwa na kurudishwa na wengine ambao mpaka leo familia zao hazijui wako wapi lakin yote hayo Tulia Akson hakuyaona.
Siku kadhaa nyuma CHADEMA waliitisha mkutano huku wakiwaalika waliopotelewa na ndugu, wenza na watoto wao kufika na zaidi ya watu 20 walitoa ushahidi wa kupotelewa/kutekwa kwa ndugu zao huku wakiomba serikali iwasaidie kuwapata. Hayo yote Spika Tulia hakuyaona.
Najua kawaida ya Binadamu ni kwamba huwa hatujui maumivu yake mpaka yatupate au yampate ndugu zetu wa karibu.
Siku kama nne nyuma zilisambaa taarifa za kutekwa kwa Mzee Ali Kibao akiwa kwenye basi kuelekea Tanga. Taarifa zilisema alitekwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi huku wakiwa wamebeba silaha za vita na kuondoka nae kisha siku mbili baadae mwili wake ukaokotwa ukiwa umemwagiwa tindikali.
Hapa ndipo Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan kutoa salam za pole kwa familia na ndugu wa Marehemu Mzee Ali Kibao wa karibu katika mtandao wa X huku akiambatanisha na Picha ya mkutano.
ndipo Spika tulia nae akapost katika mtandao huo huku akisema amesikitishwa sana na kifo hicho kilichotokana na KUTEKWA NA KUULIWA. HOJA AMBAYO ALIKATAA BUNGE LAKE LISIIJADILI.
Baada ya Rais kuona ndipo nae sasa Spika Tulia Akson akaona
Binafsi sikuwa na mfaham wala sijàwah mfaham huyu mzee labda kwa sababu sifatilii sana mambo ya siasa ila mauaji yake yamenisikitisha sana. Kwanza kwa umri wake lakn pia ameuliwa kikatili mno na kumwagiwa tindikali mbali na kwamba sio watu ambao labda walikuwa mstari wa mbele kuikosoa na kuisema serikali mtandaoni hasa X.
Hapa nawaza;
1. Je Spika Tulia ana mtoto? Kama anae, mwanae angepotezwa kama Chadrack angeendelea kusimamia msimamo wake kuwa tusitumie hisia?
2. Je mm na ww ambao hatuna cheo chochote tukitekwa/kupotezwa itakuwaje?
3. Je kuna uhai wa mtu ambao una thamani kuliko wa mtu mwingine?
4. Je Bunge litajadiri haya au ndo bado tusiendelee kutumia hisia??
5. JE NANI ALIYE SALAMA?
Naandika haya nikiwa na nia njema katika Taifa hili, Hizi damu za watu zinazopotea hazitaenda bure.
Huenda wanaotekeleza haya wapo humu au wanafanya kwa KUJIFURAHISHA AU KUMFURAHISHA MWINGINE/KIONGOZI /VIONGOZI wao. Je walishawahi kujiuliza baada ya hapa itakuwaje??
WATAWEZA KUYAJIBU HAYA KWA MWENYEZI MUNGU??
Ina maana asahv watu tumekuwa wanyama kiasi hiki na kujipa mamlaka ya Mungu ya nani aishi na nani afe na kwa muda gani??
Polisi ambao lilikuwa ndo kimbilio letu hawajatoka kukanusha kuhusika na kifu cha Mzee Ali Kibao.
Wana uwezo wa kutuua lakini laana itawaandama, familia zetu na watoto wetu hawatowaacha salama.
Naamini Mungu yupo na anajibu, UZURI WOTE MPAKA MWAKA 3010 TUTAKUWA TUMEKUFA.
Mwisho Kabisa.
Natoa Rai kwa Spika wa Bunge la JMT kujadili hoja hii ya watu kutekwa, kupotea/kupotezwa na kuuliwa. Kwani zawadi ya uhai tumepewa na Mungu na hakuna mwenye mamlaka ya kuipora.
Mungu ibariki Tanzania!
Pia soma:

- Spika Tulia: Tusiweke mazingira ya kuonesha kuwa kila anayepotea amechukuliwa na Vyombo vya Dola. Tusitumie mihemko
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Kuelekea 2025 - Spika Dkt. Tulia na Wabunge wa CCM wagomea hoja ya watu kutekwa na kuuawa kujadiliwa. Wananchi Tuwaambie "YOU ARE FIRED"