TensorFlow
JF-Expert Member
- Feb 11, 2020
- 993
- 1,286
Wakuu,
Watu kutoka manispaa za Kinondoni na Temeke wamekuwa na hekaheka za kwenda kwenye sehemu za wafanyabiashara, maarufu kama fremu na kupima mabango ambayo yapo kwenye sehemu za biashara, na kudai yalipiwe. Hizo ni sheria za manispaa.
Najiuliza sana, kuwa bango lengo lake ni kuelekeza wateja kuwa kuna huduma fulani sehemu, wakishapata huduma hiyo, mwenye biashara analipa kodi na maushuru kibao serikalini, chahce tu ni kodi ya TRA, service levy - halmashauri husika, leseni, withholding tax, kodi ya pango, tozo kibao, usafi, nk.!
Sasa hapa inategemea na aina ya biashara, zingine zina msururu wa kodi na ushuru na vibali mpaka unajuta!
Huu ubunifu ni wa serikali yetu, mtu binafsi au ni nini hiki?
Kama bango lipo eneo la serikali, mfano yale makubwa barabarani kulipia sikatai, lakini bango lipo exactly sehemu yako ya biashara na tayari unalipa kodi na maushuru ya kufa mtu!
Mbona tunaua biashara kwa makusudi?
Tujadili.
tf.