'Nimeshikwa, nashindwa kujinasua, hebu nisaidieni'

as long dini yako inaruhusu wake zaidi ya mmoja-unaweza kumchukua huyo binti jumla
 
Swala la kuoa mke wa pili unajidanganya, unatakiwa uwe muadilifu kweli kweli vinginevyo mzee umekwisha. Muda si mrefu utatembelea ndala, kuna wenzako walijidanganya kwenye nafsi zao huku wakisingizia dini lakini chamoto wamekiona. Someni dini vizuri mtaelewa maana ya mke zaidi ya mmoja.
 
Wewe si muislamu..Oa wote bana..eeeh .Dini yako inakuruhusu
 

I feel very bad for what you have done to your wife!
Nenda ukamuombe msamaha haraka sana kakangu, Kilio anacholia mkeo na sala anayoiomba sijui kama utakuja kufanikiwa maishani mwako. Wengi wenu huwa mnatumia kigezo cha dini kufanya uzinzi wenu lakini si halali kamwe. Imagine kama mkeo angekufanyia hivyo ungejisikiaje?. Sio vizuri mkuu!
Wakumbuke pia watoto wako ukimchukua huyo hawara hawezi kuwahudumia vizuri kama mama yao angewahudumia, maisha yenyewe haya magumu ndo unataka kuwapanga hao wake utaweza?
 
as long dini yako inaruhusu wake zaidi ya mmoja-unaweza kumchukua huyo binti jumla

Dini sio kigezo cha kufanyia uzinzi na kumletea dharau mkeo wa ndoa, Naomba mkasome sheria "zenu" vizuri kama zinaruhusu hadi mke wa ndoa kupigwa na hawara na kuletewa dharau za kijingajinga. Kama zinaruhusu hayo sidhani kama inatenda haki itakuwa ni unyanyasaji tu!
 
Tabia haina dawa,huyo kaka ni mzinzi by nature! Binafsi fikiria kama mkeo nae angekufanyia unayomtendea! Dont' be selfish elewa kuwa unamuumiza mkeo wa maisha.
 
Sikiza wewe baba alichofanya huyo binti cha kumpigia mkeo is very nice

cz asingejua mambo yako unayoyafanya, naisitoshe unavomwambia unataka kuoa mke wa pili kisa dini inaruhusu

mbona hukumwabia mke wangu sasa hv natoka nje, kuoa mke wa pili kwa kisingizio cha dini ni kujikosha kwa mkeo kuonekana ww ni muwazi kumbe......lol?

kumbuka MSHAHARA WA DHAMBI MAUTI
 
Pole. Huna jinsi. Ongea vizuri na mke mkubwa ukimuomba radhi na kumweleza hali halisi ilivyo ukimuomba radhi akusamehe kwa dhambi ya uzinzi. Muombe akubali uoe mke wa pili kwa kuwa dini yako inaruhusu ila hukuwa mwaminifu tangu mwanzo. Akikataa kata kata, itabidi uachane na huyo binti.
 
Mzee mwenzangu mi naona hawa watoto huku wanakuzingua tu, ngoja nikupe mbinu...

Muache tena kwa mda huyo mdada, alafu wakati ukiwa hauko nae, akili itafikiria cha kufanya, japo kwa uzoefu wangu hutaweza kumuacha jumla.

Namna ya kumuacha; Wanawake (nyumba ndogo), wapo tu kwa ajili ya hela zako. Sasa wewe mdanganye kuwa kuna tatizo kubwa limetokea (mfano umeingiza hasara kazini), na hivyo karibia mshahara wako wote unakatwa. Kuanzia hapo punguza kutoa matumizi kwa asilimia 95, lakini ukijifanya bado unampenda sana. Kwa kweli siku si nyingi huyo mwanamke atatafuta kisingizio cha kukupiga chini, na wewe utapata mahala pa kuchomokea, maana atakuwa amekuuzi...
 

Punguza mikwara...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…