Ukiweka Nia ya dhati.
Unaweza ukaacha au ukapunguza kwa kiasi kikubwa.
Hebu jaribu mbinu hizi;-
1. Wakwepe hao marafiki.
Ni ngumu ila fanya tu namna uwakwepe.
2. Kwakuwa kuacha moja kwa moja ni ngumu. Bas anza kwa kupunguza siku za kunywa. Kunywa Ijumaa na Jumamos tu, na sio kila siku.
3. Ule Muda ukitoka kwenye harakat. Badala ya kufikiria kwenda bar na kujipongeza . Tafuta kitu kingine ufanye. Either mazoezi. Kusoma vitabu. Gazeti. Kuwapigia simu ndugu na jamaa. Kufuatilia mipango yako ambayo unahisi haiendi kwasababu ya muda. Nk nk
Yaani hakikisha unakuwa busy yale masaa ambayo unaendaga bar.
Alaf ww ni mwanamke, ukitoka harakat, rud home haraka kapikie familia.
4. Hela ile ya kunywa bia , itunze au either ununulie kitu ambacho utapeleka home.
Ukiwa na tabia hii, kuna siku utaona vitu ulivyonunua na ukajishukuru kwa maamuz ya kununua vitu na sio hela kuinywea. Na hivyo itakujenga kiakili kuwa bia sio za kuendekeza au za kunywa mara kwa mara.
Kila la kheri.
Mm nilifanikiwa kuacha kwa miez 3.
Nikarudia kunywa ila Sikuhizi Mind yangu iko strong na inazid kuimarika.
because nakunywa ijumaa au jumamosi. Tena bila kampan.
Na naenda na budget fixed kabisa.
Na niliweza kupunguza kwa kureplace ule muda wa kwenda bar kwa vitu hivyo hapo juu.
Be blessed na kila la kheri.
Ila bana kama ww ni mchaga , pombe iko ndan ya damu, kuacha itakuwia vigumu sana [emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji3526][emoji3526].
Sijawah ona mchaga akawa mnywaj alaf akafanikiwa kuacha. Labda aumwe na ameze dawa kila siku.
Sent from my Infinix X657B using
JamiiForums mobile app