0713417189
Senior Member
- May 12, 2021
- 115
- 201
NIMESHINDWA KUISHI KWA MAKOSA YANGU MWENYEWE.
Lovi Pius Kijogoo
0757 238 304 ( WHATSAAP )
SEHEMU YA KWANZA.
NYAKATO KWA SAA NANE SOKONI.
"Karibu dagaa safi kabisa. Nguo unapata kwa shilingi elfu moja tu, ni sawa na bure. Kula madagele ya leo leo ukichelewa hupati kitu"
Hizo zilikuwa ni sauti za wafanya biashara mbali mbali wakinadi bidhaa zao. Katika soko maarufu mjini Musoma. Naam, wanapaita Nyakato, mtaa huo ukiachilia mbali soko hilo. Ni maarufu sana kwa uuzaji wa pombe za kienyeji hasa gongo.
Wakazi wake ni wengi sana. Pamechangamka. Watu kutoka kijijiji jirani cha bisumwa wamekuwa wakinyonga baiskeli zao kufata mahitaji muhimu. Kwa yeyote aliyewahi kuishi manispaa ya Musoma mkoani Mara, anaujua vyema umaarufu wa mtaa huo. Hasa miaka ya nyuma kuna kundi la vijana waliokuwa wakipora mali za watu. Walitumia eneo hilo kama maficho yao.
Vumbi jekundu, tope wakati wa mvua havikuweza kukwepeka. Katika medani za siasa hawakuwa nyuma. Nyakati za uchaguzi chama tawala kilikuwa kikikutana na upinzani mkali. Kutoka katika chama cha CHADEMA. ofisi za Chadema zilikuwa huko nyakato.
. Chezea Nyakato wewe, ni uswahilini penye kila burudani uliyohitaji. Makazi mengi yalikuwa ni duni. Na kabila lililokuwa na watu wengi hapo ni wakwaya na hata wajita pia.
Kelele za watu kuibiwa nyakati za usiku. Hapo ndipo palikuwa nyumbani kwake. Nani atoke pindi asikiapo yowe. Waliogopa, waliishi hivyo mpaka pale serikali ya mtaa ilipoamua kulivalia njuga. Vikao vya kila mara vikatokomeza kwa kiasi fulani tabia hiyo. Lakini katika suala la vijana kubwia pombe za kienyeji asubuhi, lilishindikana. Walipokamata wauza gongo kwa wingi. Vijana hao wakaamia kwenye pombe kali za kupima. Mtanange ukazidi kupamba moto.
_____________________________________
PAULINA alikuwa ni binti wa mzee maarufu sana hapo nyakato. Katika maeneo ya magamaga. Ni binti wa mzee Makunja Maregesi. Ukiuliza hata mtoto wa miaka mitano akupeleke katika mji huo, basi ondoa shaka umefika bila ya kupotea. Ucheshi, hekima na hata busara zilichagiza kufahamika kwake.. Lakini pia alikuwa ni fundi baiskeli wa miaka mingi sana. Uaminifu wake ukamuongezea wateja wengi. Na kufanya familia yake iweze kupata mahitaji ya kila siku. Kwa kile kidogo kilichokuwa kikipatikana. Ule upara wake kichwani ukamuongeza jina la utani kwamba mzee kipara. Hakuwa na hiana akalipokea kwa mikono miwili.
Nyumbani kwake alifanikiwa kufuga mbuzi wawili, ambao waliongezeka mpaka kufika watano. Kadiri siku zilivyozidi kwenda uzee ulimtafuna. Na hapo ndipo akajilaumu kwa kuchelewa kuoa na kupata watoto. Nguvu za kugongelea vyuma vya baiskeli, hatimaye zilianza kupungua. Ugonjwa wa kibofu cha mkojo ukawa pigo kwake. Na kudhoofisha kabisa utafutaji wake. Maisha yakazidi kuwa magumu. Mkewe ambaye hakuwa na umri mkubwa. Akayavaa majukumu na kuanza kuuza dagaa wa bichi katika soko hilo la Nyakato.
Kupanda kwa bei ya nyama. Na samaki aina ya sato na sangara kuadimika. Ilikuwa ni furaha kwa wauza dagaa. Kwani familia nyingi za Musoma ziliweza kumudu kununua dagaa kuliko nyama. Mkewe Mzee Makunja, akamshukuru Mungu. Kwani pesa aliiona na kuanza kuweka akiba, ambayo ikawa inamsaidia mumewe katika matitabu. Lakini kauli ya madaktari kwamba Makunja anatakiwa apelekwe hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Kwaajili ya upasuaji mkubwa. Ilimuumiza sana Mama huyo. Pesa aliyokuwa nayo isingefua dafu.
______________________
PAULINA alikuwa ni mtoto wa pili na wa mwisho wa Mzee Makunja. Kakake hakuwa na muda mwingi Duniani. Alifariki akiwa na miaka ishirini tu. Aliitwa Machumu. Alibahatika kumaliza kidato cha nne katika shule ya sekondari Mshikamano. Iliyopo hapo hapo manispaa ya Musoma Mjini. Matokeo yalikuwa mabaya kwake. Alipata daraja sifuri kabisa. Hakujutia hata kidogo, kwani kwa mwezi alihudhuria shuleni mara tano au kumi. Wazazi waliongea na kumkanya lakini hakuskia. Majuto ni mjukuu, msemo huo kwake haukuwa na maana kabisa.
Machumu kabla ya umauti kumfika. Aliamua kuwa boda boda wa pikipiki. Alikuwa anapaki hapo kwa saa nane katika soko la Nyakato. Pesa ya kula na hata kuwapelekea wazazi wake Furu, madegere, na unga havikumpiga chenga. Akaanza kuwa anawapiga vijembe wale waliosoma mpaka vyuo vikuu na wapo tu mtaani. wakitegemea wazazi wao kwa kila kitu.
______________________
ITAENDELEA........