Nimeshindwa kuuthibiti wivu

Hata mimi nina wivu sana kwa mahondaw wangu... Siku zingine najikuta mnamgombeza, au nachukia kwa vitu vidogo sana... basi tu najikuta hivyo... But najitahidi sana to stay cool, calm and positive inasaidia sana...


Cc: mahondaw

Uwiii hapo kwenye wivu hapo dahhhhhhhhhhh
Mimi ninao uliopitiliza kabisa kwa Smart911 teinaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lol Naachaje kuwa na wivu kwa mwanaume mzuri mtamu hivi??

Unisamehe tu Smart911 I love sanaaaaaaaaa as
 
Hongera kwanza kwa kujua tatizo lako. Wivu kwenye penzi ni lazima uwepo ila ukipitiliza huwa ni kero kubwa na kuondoa amani ndani ya penzi. Kuwa na SUBIRA Mkuu badala ya kuanza kumfikiria mwenzio vibaya.

 
» Jitahidi kuwa positive kwa huyo mpenzi wako, usifikirie ubaya/dhambi juu yake.

» Jichunguze wewe kwanza, una insecurity zipi kwa huyo mpenzi wako? Humridhishi kimwili, kiuchumi au hata maisha ya kijamii kiasi kwamba unahisi kuna mtu anaweza kumtimizia hayo mambo?

»Katika life lako je, unaweza kutawala hasira, huzuni, hisia zako? Kama sivyo jiangalie na jitahidi kujitawala, it all begins with you, in your brain. Control yourself bro.

» Lakini pia, usitumie mda mwingi kumuwaza huyo mdada kiasi kwamba unspoteza focus ya maisha binafsi. Be a little selfish, love yourself, ukiona jambo hulielewi we potezea na umtafute some other time.

Wivu ukiuendekeza utakuletea maradhi ya shinikizo la damu na sukari mwilini.
 
Piga moyo konde kwa kutuliza hisia zako unapokuwa na wivu unao kukamata.Jaribu kutambua mzizi wa hisia zako.
 
Endelea kujiona mpuuzi hivyo hivyo utashinda
 
Wivu ktk hali halisi ni uoga wa kupoteza mtu au kitu fulan.Wivu huenda sambamba na hasira kwamba mtu fulan ana tumia mali yako...

Fanya juu chini utambue fikra zinazo kutuma kuwa na hisia za wivu,badala yake fikra hizo zifute na kupanda fikra za kujiamin

Kikubwa umwamini tuu
 
Ama kweli wivu kidonda,Ukishiriki utakonda. Pole mkuu
 
Kaka, kuhusu wivu ni kwamba , "wivu" ni kipimo cha mapenzi baina ya wapendanao, wivu upo na lazima uwenao kwa yule unayempenda kwa dhati, hata ukisoma kwenye kitabu cha Mambo ya Walawi utaona kuwa wivu unaruhusiwa ila ukizidi mhusika lazima atapata adhabu maana atakuwa anahatarisha usalama wa mwenzi wake.
Kaka ushauri wangu ni huu, unampenda mpenzi wako, mwamini na kumtia moyo kila wakati kwa tabia nzuri ya uaminifu aliyokuwanayo.
Kwa kufanya hivyo utaweza kuudhibiti wivu juu ya mpenzi wako.
Siku zote muwazie mawazo mazuri na ya mafanikio mpenzi wako kwa kufanya hivyo utakuwa na amani sana moyoni mwako juu ya mpenzi wako.
Nakutakia kila la heri kwenye penzi lako.
 
Pole sana. Wivu ni ulemavu mbaya kuliko hata ule ulemavu wa ngozi au ule wa kuwa kipofu, kiziwi au hata kukatika miguu yote miwili... Wivu ni kutitesa mwenyewe kihisia... By the way hao madem uliwakuta bikra? Kama uliridhia kuwa na dem used amini kuwa lolote laweza kutokea pia...
 
Yawezekana ww sio mwaminifu just why humwamini mwenzako. Ila chukulia kila anachokwambia ni cha kweli usijaribu kuchimbachimba
 
Nashindwa kukushauri kwa kuwa kichwa cha habari sijakielewa. Maana siku hizi watu wanachanganya kati ya neno KUDHIBITISHA na KUTHIBITISHA.
Kwanza kudhibitisha sidhani kama liko kwenye kamusi,neno sahihi ni kudhibitisha maana yake kuhakiki.
kudhibiti ni maana nyingine kabisa, maana yake ni kuweka katika himaya.
 
Kaa na mweleze mpenzi wako kuhusiana na tabia yako ya mawivu ili ikitokea akupuuze.

Mfano mimi ni mtu wa mahasirahasira na kisirani katika mapenzi hasa kwa nnae mpenda.nilishindwa kuizibiti tabia yangu nikakuta sidumu na wanawake.mana wanawake wengi mwanzo wananionaga kama mpole.unakuta toka mwanzo namwambia kama nna masihara anachukulia ni utani.mbele ya safar wanakuja kugundua ni kwel wanaamua kunizoea na wananpuuza

Mfano huwa mara nyingi nawahusisha kwenye dili za pesa.sasa kuwe na dil achelewe dk 5 ni ugomv siku nzima.20000+2450000+30000+100000=anahesabu vidole akili imelala ugomv,hana maamuz ya haraka ni ugomvi na kufokaga kwa hasira.akidanganya mda akachelewa ghetto nmesusa.

Kila mtu na mapungufu yake
 
When you want something,it costs more..solution ndogo jichanganye ume invest sn kwenye mapenzi na si ajabu hata urafiki wa kawaida na wadada wengine huna kisa una mpenzi unampenda,pili kusalitiwa kupoooo accept the fact,tatu kwa wahuni ndo tunakuwaga na kamchepuko kamoja kwann wanaunme wanapenda michepuko hili ndo jibu kati ya mengi...mwanaume mwenye mchepuko anakuwa sio insecure km wewe sababu anakuwa ana other options...hamna kitu kibaya km kuwa mwanaume halafu huna options hii inawashinda wanaume wengi ndo mana wanaamua kuwa na mchepuko ila kubalance personality ya kiume amabyo inakutaka ww km mwanaume kujiamini kitu ambacho ni kazi sn km una wivu...huna hobby pia na you are over sensitive ni kama ni over sensitive basi hata story za humu khs mtu kumsaliti mwenzake HUPASWI kusikia kila siku sababu zinazidi kukutia uoga..
 
bora wewe.. mi mwenzio nikiona mke wangu anakaa sana kwenye kioo naenda kukichungulia usikute kuna mtu wanaongea...!!!!
wivu kiboko...!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…