Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,925
Hii ni dalili kwamba Tanzania hatuna sheria ya kutetea haki za watoto. Maandamano ya hawa watoto au wanafunzi hayakuwa uvujaji wa amani au sheria, bali kuisaidia serikali kufungua zaidi na kuona madai ya walimu yafikiwe mwafaka ili wasiendelee kukosa vipindi madarasani sababu ya mgomo wa walimu.
Askari polisi kutumia silaha za kivita kutishia uhai wa wanafunzi ni jambo hatari kabisa kwa malezi ya watoto hawa, la ajabu, na lisilo la kistaarbu kabisa, na kabisa kisaikolojia ni kuwaharibu hawa watoto. Athari za matukio ya polisi kutishia watoto kwa silaha kali za kivita ni kubwa katika maisha yao, na hapo ndipo busara inapokosekana kwa serikali na jeshi la polisi nchini ni kielelezo tosha.
Tanzania hatuna wanasaikolojia wanaoweza kuwasaidia hawa watoto kuongea nao wakaelewa na pengine wakachukua mawazo ya watoto hawa na kuyafanyia kazi, na badala ya watoto hawa kuwatisha wanafunzi uhai wao ka mitutu ya bunguki na mabomu ya machozi, je walikuwa na silaha gani kama si mikono mitupu kudai haki yao ya kupata elimu jambo ambalo linaeleweka kwa kila mmoja? Wizara ya jamii na watoto kazi yao nini , na wanafanya nini kutetea hawa watoto?
Hawa watoto ni haki yao kudai muda unaopotezwa na walimu wanapodai haki zao wakati wanakosa masomo madarasani. Binafsi sioni kosa la watoto kama maandamano yao yalikuwa ya amani, na kama waliziba njia ni bora kutumia njia za kisaikolojia kuwatuliza wanafunzi kuliko tishio la silaha za kivita.
Serikali iko tayari kusikiliza kilio cha wanasiasa wabunge kuwaongezea mishahara na malupulupu, lakini wanaosota maisha yao yote kuandaa hili taifa la kesho wamewapiga danadana siku nyingi na leo wanapochukua hatua serikali inaamua kumalizia hasira kwa hawa malaika wasio na makosa, waadhiriwa na mgomo wa walimu.
Je, serikali inapotumia jeshi la polisi kutishia watoto hawa ambao ni waadhirika wa kukosa masomo bila ridhaa yao kwa uzembe wa serikali yenyewe, je inajengwa taswira gani katika maisha, malezi na future ya watoto hawa?
:nono:Hili ndilo tatizo la vyombo vya dola vinapotumika zaidi kisiasa.:nono: