milionea wa kesho
JF-Expert Member
- Dec 28, 2015
- 328
- 631
Kwa wiki nzima sasa nimezunguka vijiji kadhaa nikifanya ziara ya kitafiti kuhusu kilimo. In fact tusiite ziara niseme tu nachunguzachunguza mustakabali wa kilimo kupitia kivuli cha kuwatembelea ndugu zangu wajomba na mashangazi vijijini huko ndani ndani.
Asikuambie mtu kilimo kinalipa. Majority ya wakazi wa kijijini niliofanikiwa kukutana nao wanalima small scale agriculture kwa kutumia jembe la mkono na ni kilimo local sana.
Ajabu ni kwamba watu wanaendesha maisha yao vizuri kabisa. Kuna vijana wa rika langu ambao wakati mimi nafaulu vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari, wao hawakubahatika hivo wakalazimika kubaki kijijini kulima.
Leo nimekutana nao wana maisha mazuri kwelikweli. Wote wamejenga nyumba zao. Unaweza kusema kujenga kijijini sio gharama kubwa. Lakini hawa vijana wametumia tofali za block kama mjini, nyumba zao zina dirisha za aluminium na wengine tiles kabisa. Vijana wengine kadhaa wamemiliki gari zao nzuri tu kama Toyota Noah na malori. Bodaboda ndo usiseme zipo nyingi.
Kuna jamaa mmoja tulisomaga naye shule ya msingi alikua kilaza kweli. Karibia kila mtihani alikua wa mwisho. Ni mtu aliyedharaulika mno. Leo nikakutana naye dukani kwake tukawa tunapiga stori. Ana mke na watoto. Amejenga nyumba nzuri. Pia ana Toyota Noah namba D mpya kabisa rangi nyeusi. Akaniambia mafanikio yote hayo ni kilimo na analima kilimo cha kienyeji. Sasa mimi niliyekuwa masomoni nikijiangalia sina hela naona aibu japo inashauriwa usijilinganishe na mtu bali jilinganishe wewe wa jana na wewe wa leo.
Sasa nimekaa nikatafakari kama hawa wakulima wa kienyeji wanapiga hela hivi, vipi akienda mtu alime maeneo yale yale kwa kilimo chenye tija? Alime kwa kufuata taratibu zote za kilimo? Si atatoboa upesi sana?
Wakulima wazoefu mkuje huku kutuambia kama kilimo kinalipa au la. Maana nilichokiona leo kimenitia nguvu sana nikalime.