Nimesikia Bi Khadija Kopa anataka kuununua ugomvi kwa bei yoyote: You have my support

Nimesikia Bi Khadija Kopa anataka kuununua ugomvi kwa bei yoyote: You have my support

Judi wa Kishua

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2012
Posts
1,159
Reaction score
1,274
Bi Khadija ndio msanii wangu pendwa wa muda wote, toka enzi za TOT tunavimba nae. Mwananyamala bi Khadija hana shida na mtu yeye ni mpole si chakaramu kama umuonavyo jukwaani alikuwa vizuri na kila mtu. Muulizeni marehemu Nasma. Khadija mnamuita mama kwetu wengine ni dada tena gwiji haswa. Yoyote ataemkera ajue anaturudisha kwenye ujana hatutokubali. Bi Khadija ukinunua ugomvi tuuzie hisa na sisi tunautaka.
 
Nje ya mada: Dah, umenikumbusha Bi Nasma. Yani taarabu ilikuwa enzi zile, yani chambo chambo la maana.
Enzi za sanamu la Michelin, y2k, etc.
Hawa wamama walijua kutuchangamsha na maisha ya kiswahili.
Baada ya kufariki Nasma, bi Khadija alijaribu kumjibu utalijua jiji ila kwangu niliona iko low sio kama enzi zake na Nasma.
 
Mwananyamala bi Khadija hana shida na mtu yeye ni mpole si chakaramu kama umuonavyo jukwaani alikuwa vizuri na kila mtu.
. Yoyote ataemkera ajue anaturudisha kwenye ujana hatutokubali. Bi Khadija ukinunua ugomvi tuuzie hisa na sisi tunautaka.
😂😆😀 hisa tena. Umejua kunichekesha. Anza na mai, Nina hakika utammudu 😀
 
Aah, we Dada Judy weeee, umenipa mzuka usikuusiku yani umenivurugaaa. Medulla imehamia mbele. Nilikuwa napenda sana vile vibwagizo sijui vianzio.
Yani kama kile cha muungano.
(Muunganooooo hatarii, imemtoa mwanamwali juu ya dari, anaetaka kuja je? Tafadhali, na hasiyetaka kuja je? Don't worry about kujali) 😄😅😆😆
Alafu kuna ile walijibiwa baada ya kuimba achia ngazi bibi mchuma unaondoka huo......
Jibu(mchuma huo unapitaaaaaa.....na upite, hatupandi mchuma unaokwenda mwanza siku 3, tunapanda jet, inayokwenda mwanza dakika 3, heheheeeee mambo ya fedhaaaaa)
 
Bi Khadija ndio msanii wangu pendwa wa muda wote, toka enzi za TOT tunavimba nae. Mwananyamala bi Khadija hana shida na mtu yeye ni mpole si chakaramu kama umuonavyo jukwaani alikuwa vizuri na kila mtu. Muulizeni marehemu Nasma. Khadija mnamuita mama kwetu wengine ni dada tena gwiji haswa. Yoyote ataemkera ajue anaturudisha kwenye ujana hatutokubali. Bi Khadija ukinunua ugomvi tuuzie hisa na sisi tunautaka.
Sasa huyo marehemu Nasma tunamuulizaje mtu kishakufa? Ila hapa Bi Khadija kachemsha mno, mwanaye ni zezeta wa mapenzi, mtu hatakiwi lakini bado analazimisha tu maana dalili zote za mwanawe kutumiwa zinaonekana lakini mtoto kawa kiziwi na kipofu ghafla. Hapa wala asinunue ugomvi, akae chini na mwanae na kumchapa viboko mpaka akili imrudi la sivyo atajikuta anagombana na taifa zima la Tanzania kwani mwanae anakera mno na watu wanamsema kwa sababu wanamuonea huruma. Bi Khadija asipoangalia huyu mtoto atakuja kujiua mapema kwa kujinywea sumu au kujipiga kitanzi.
 
Sasa Marehemu tutamuulizaje wakati alishazikwa kitambo
 
Wazee wa nchi hii wamekosa busara kabisa, na hii ndio sababu watoto zao nao ni vijana wa hovyo tu.
 
😀😀😀🤗🤗 we da Judy weeee, natamani ka nikusimulieee afu nikusimulie tena. Nimelia sana aisee, hivi nitazitoa wapi hizi nyimbo.
Hazipo youtube,boomplay,audiomack na kwenye platforms nyingine
 
Kama ni suala la mwanaye makosa ni yake kama vile justin beiber, na ulsher raymond wazazi wao walivyowakabidhi kwa bwana pdiddy
 
Alimjibuje marehemu
Utalijua jiji haikuimbwa na marehemu nasma. Iliimbwa na East Africa melody nadhani, na khadija kopa aliijibu kwa kuimba nalijua jiji.
Nadhani hukuwa umenielewa nilichomaanisha. Ilishazoeleka vijembe ni nasma na khadija, ndio maana nikasema alipofariki nasma, khadija aliijibu utalijua jiji lakini haikubamba kivile

Ok nimekupata
 
Alisikika binti wa manzese. Binti wa magomeni. Binti wa buza akifloow na bit la kusaula
 
...nimezaliwa ocean road.
Na hii nayo si ilijibiwa na Banza stone
Eeh, ndio nakusika. Alimjibu banza kivipi? Mimi kwenye umbea wangu sifahamu hivyo. Maana nalijua jiji bishoo najua ilijibiwa ea melody.
Nipe hiyo story ya banza, ndio nakusikia wewe.
 
Back
Top Bottom