Nimesikia mbunge akisema eti anawashangaa Wanasheria katika kesi ya Tundu Lissu

MwajabuOmary

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
2,059
Reaction score
2,982
Kama anawashangaa wanasheria vivyo hivyo na wao wanamshangaa kwa kushindwa kujenga hoja na kuleta hisia zake za nyumbani.

Na nimshauri tu kwamba kaa mbali na hao watu, jamaa wakitoka arusha wakikuwashia moto utatafuta mlango wa kutokea.

Unaweza kuwa Mbunge lkn usijue hata principles za makosa ya uasi, unaweza kuwa mbunge lkn usiweze jua hata principle mbili za kosa la uhaini.

Wenzako hizo principles wanazo kwenye vidole na ndio maana wanachokisema wanakijua. Msikulupuke kuwadanganya watanzania.

Eti anawashangaa.
Na sisi pia tunakushangaa
 
Mbali na babu tale aliyeuliza swali la nyongeza kuwa "Ni lini serikali itashirikiana nae kuleta mkandarasi wa finance and building"
Kuna mbunge mwingine wa viti maalumu, aliwai kutoa hoja kwamba anaiomba serikali itengeneze chombo maalumu huru, cha kuisimamia serikali

Nilichoka🤣🤣🤣
CCM shkamoo
 
😂😂😂😂😂
 
Lkn yule mwanasheria mkuu wa chadema kuongea ktk media hawezi
 

Mkuu una muda wa kuwasikiliza hawa chawa wa jiwe? A ana be wanazijua? Rubber stamp tu ya kupitishia mboga toka sisiem
 

dunia nzima haijawahi kutokea kwa mtu mmoja tu yeye pekeyake kushtakiwa kwa kosa la uhaini.
Uhaini hauwezi kufanywa na mtu mmoja tu ndio maana hiyo kesi inaonekana ya kisiasa zaidi.
Ukielewa Zana nzima ya uhaini treason ndio utaelewq
 
Hapa ndio utajua makosa ya mihimili kutozingatia Sheria kwa kujua au kutojua!
 
Naona kama baada ya mtu kutangazwa kuwa ameshinda nahisi kuna nyuzi huwa zinakatika, kwa sababu katiba na sheria ziko wazi juu ya majukumu ya mbunge. Lkn kwa sasa tulipofikia huwezi jua huyu ni mbunge au ni mkuu wa wilaya, au ni waziri, yaani mimi naona kama ni kitu kimoja. Ukisikia luga gongana ndio hapa tulipo. Ninachojua mimi ukiwa kiongozi lazima uchague cha kusema kwa wananchi na sio kuja na maneno yako.
 
Sijajua niite kituko, au kichekesho au ndio utaratibu, anaetaka kuajili wajeshi ni CDF, kwa nini anataka waliopitia mafunzo ya JKT ni yeye ndio anajua, sasa, bunge linampangia CDF watu wa kuwaajili. Do you no his budget, huenda amefanya hivyo kupunguza muda wa mafunzo kulingana na budget yake ndio maana ameamua kuchukua walio na taaluma za kijeshi lkn kwa kuwa wao ndio kila kitu CDF wait tukuletee sifa za waombaji. Du!
 
Usipochagua maneno ndio utaishia kusema chadema wanaleta ebola, na sijui ile barua waliyomwandikia imeishia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…