Nimesikiliza mahojiano ya Prof. Assad na Kikeke, huyu Prof. ana ujuaji mwingi. Unafukuzaje mfanyakazi akikataa kufanya majukumu ambayo sio yake?

Labda anajutia alichopanda!
 
Majukumu 1,2,3 pamoja na majukumu mengine.Hivi mnaelewa hivi vipengeleee amaaa?
 
Nae analia lia mno alitaka afie kwenye ofisi
 
Ila mikataba ya kazi pia inampa room kumpangia mtumishi majukumu mengine na mtumishi anapaswa kuyafanya provided that hayamdhalilishi.
Ni majukum mengine lakin lazime yawe na uhusiano na taaluma yake
 
Mi nadhani nyie wengine endeleeni kufanya kazi serikalini tu; huku kwenye private sector achaneni nako kabisa. Sasa mtu ni dereva, gari la kuendesha halipo, mtu wa kumuendesha pia huna so kazini unakwenda kufanya nini? Kwamba kupanga mafaili nayo unaona ni kazi ya kukataa? Mfumo wa ujamaa umetulemaza sana Watanzania. Niliwahi kuajiriwa kampuni moja kubwa ya kigeni; mkurugenzi aliwahi tamka hivi, "duniani (akiwa na maana makampuni kama la aina ile) hakuna kazi inayoitwa UDEREVA, everybody should drive his own car, I drive myself from home my office, from my office back to home" wakuu wengine nao wakalazimika kuanza kujiendesha wenyewe, hadi naondoka pale, madereva walikua 3 tu but walikuaga wanafanya kazi zingine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…