Nimesikitishwa na hiki kitendo, kweli sasa naamini Dunia imebadilika!

Nimesikitishwa na hiki kitendo, kweli sasa naamini Dunia imebadilika!

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nimeshangaa wamasai wanalia. Wamasai wanalia Sabaya aachiwe! Hii inashangaza. Zamani hili jambo lingeitishiwa kikao na Maleigwani huko kwao.

Mmasai anatakiwa apandishe Mori siyo kulia. Miaka hii Mmasai analia? Wamasai walikuwa walinzi miaka yetu walinzi wa kuaminika. Sasa hivi wasusi, Daaah. Inaumiza sana. Kutoka kwenye ulinzi hadi kuwa wasusi? Afadhali wangeshuka hadi kuwa migambo. Inaumiza sana.

Wamakonde. Hawa nakumbuka home alikuwepo mmoja mlinzi.miaka ya 80's tu hapa wala si mbali. Alikuwa mlinzi na mishale yake humwambii kitu. Sasa wamakonde wanauza vipodozi. Sasa hivi huwasikii tena. "Ukisimama nchale, ukikimbia nchale, ukilala chini nchale, ukichuchumaa nchale, ukiinama nchale, ukikaa nchale".

Hamna kitu tena. Mambo yamebadilika na dunia ya sasa si dunia ya zamani.
 
Umechelewa sana kulijua hilo, wamasai wengi siku hizi midebwedo ni wauza urembo tu shanga na mikanda…. kuna mmoja huku sharobaro huwezi amini.
 
Wamasai sku hiI tuko nao disko vumbi wanacheza singeLi sio kipolepole
 
Laigwanan sio laigwani. Halafu hao wamasai feki wa hapo Chalinze na Morogoro usifananishe na Masai. Masai OG yupo Ngorongoro, Longido na Simanjiro.

Hao wengine ni ma Ormekii tu
Exactly [emoji1666] [emoji1666] hawa ni wamasai feki, tena wamepewa mshiko ili waje kulia hapo mahakamani...
 
Kuna mmasai huku anavaa cheni daimond akasome..kaweka drek utadhani mdogo wake sholo mwamba..
 
Back
Top Bottom