Nimesikitishwa na serikali kupandisha ada kwa vyuo vya ualimu

sulle23

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
230
Reaction score
14
Hatimaye serikali yapandisha ada kwa wanaosoma vyuo vya ualimu kwa zaidi ya mara mbili ya iliyokuwepo awali(grade a watalipa Tsh 300000,diploma arts Tsh 400000 na diploma science Tsh 600000)je hili mnalionaje jamani?
 
Sawa tu kwani wewe huoni maisha yalivyopanda mkuu.? Vipi vyuo vya binafsi ambavyo vinatoza ada zaidi ya milioni moja mbona husemi na watu wanasoma bila shida...!
 
Gharama za uendeshaji zimepanda ile ya awali kwakweli haitoshi tena make siyo rahisi mwanachuo umlishe,alale,aoge na matibabu kwa sh70,000 .
 
Sawa tu kwani wewe huoni maisha yalivyopanda mkuu.? Vipi vyuo vya binafsi ambavyo vinatoza ada zaidi ya milioni moja mbona husemi na watu wanasoma bila shida...!
Hakika mkuu laki tatu na laki nne kwa mwaka bado ni pesa ya kawaida uendeshaji umepanda sana hiyo gharama naona bado inalipika mbona shule za msingi kwa baadhi ya shule za binafsi watu wanalipia zaidi ya milioni mpaka mbili.
 
Sasa kwa walimu wa sayansi ada juu wakati nchi ina uhaba wa walimu wa sayansi kweli hili hamuoni
 
siemce hapo motivation inapungus
 
fair. mbona kodi za nyumba, vyakula, vifaa vya ujenzi na vyakula vyote vimepanda bei hamlalamiki
serikali sikivu inatimiza ahadi yake ya maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Ukiona Ada Ni kubwa Sana,unajaribu ujinga uko costless.
 
hahahahahahahahaha!unayesema hiyo ni sawa mimi sikuelewi maana kuna tuliosoma bure,je zile pesa kipidi kile zilitoka wapi unavosema gharama ya maisha imepanda?600000 ni nyingi sana kwa mtanzania wa kawaida,usijisemee wewe kwakuwa kwenu kuna maisha mazuri ambapo kutumia 5000 kwa cai ni kawaida.
 
Hapo ndo ucemi wa aliyenacho ataongezewa ndo mda wake pia ule wa maji hufuata mkondo maana makapuku hatutasoma.
 
wanapewa mikopo.

Wanaopewa mkopo ni kuanzia intake mpya lakn wanaoingia mwaka wa pili wanajilipia! ila serkal haikufanya haki maana apo ukijumlsha na michango utapata laki 8 hv! kwel makapuku tutasoma??
 
fair. mbona kodi za nyumba, vyakula, vifaa vya ujenzi na vyakula vyote vimepanda bei hamlalamiki
serikali sikivu inatimiza ahadi yake ya maisha bora kwa kila mtanzania.

Kodi za nyumba, umeme, vifaa vya ujenzi vikipanda tutakosa watalaam katika kada ya elimu?
 
Mlikuwa mnachukulia ualimu poa eeeeee,mbavu mjipange
 
Hatimaye serikali yapandisha ada kwa wanaosoma vyuo vya ualimu kwa zaidi ya mara mbili ya iliyokuwepo awali(grade a watalipa Tsh 300000,diploma arts Tsh 400000 na diploma science Tsh 600000)je hili mnalionaje jamani?

Mimi nilifikiri Serikali itatoa elimu ya walimu wa sayansi bure ili shule lukuki za sekondari ambazo hazina walimu wa sayansi zipate. MAAJABU KUONA ADA IMEPANDA ZAIDI HUKO. CCM INAUA ELIMU. CCM INAUA SAYANSI. CCM INAUA MAENDELEO. CCM INAUA NCHI. TAFAKARI. EWE MWANANCHI. CHUKUA HATUA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…