Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Balozi Saleh Tambwe

Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Balozi Saleh Tambwe

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SALEH RAJAB TAMBWE, JOB LUSINDE NA SAMWEL SITTA

Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Balozi Saleh Tambwe ambae tukifahamiana kwa miaka mingi na yeye akimjua babu yangu katika kundi la wazee wa Kimanyema waliopigania uhuru wa Tanganyka kutokea Tabora, Western Province.

Katika kundi hili alikuwapo Rajab Tambwe, Abdallah na Maulidi Kivuruga, Bilali Rehani Wiakela, Issa Kibira kwa kuwataja wachache.

Kiasi cha kama miaka mitatu hivi nilikutana na Balozi Tambwe Makaburi ya Kisutu akiwa ameongozana na Balozi Job Lusinde na Spika Samwel Sitta.

Balozi Tambwe akanitambulisha kwao na tukawa na mazungumzo ya hapa na pale.

Nakumbuka nilimwambia Mh. Samwel Sitta kuwa mimi namfahamu toka utoto wangu Tabora nilipokuwa nikienda likizo kwa babu yangu Baba Popo.

Jina hili ni maarufu tukawa tumefahamiana.

Lakini nikamtajia kitu ambacho naamini hakukitegemea kutoka kwangu nilipomwambia kuwa akiwa mwanafunzi alipata kushinda mashindano ya kuandika insha ya Kiingereza na zawadi yake ilikuwa safari ya Marekani.

Alifurahi sana kwa mimi kumtambua hivyo.

Balozi Job Lusinde nilimwambia kuwa nimemtaja katika kitabu cha Abdul Sykes wakati akiwa mwalimu Alliance Secondary School, Dodoma, Central Province.

Kulikuwa na mgogoro wa kuunda tawi la TANU pale mjini na viongozi wa harakati hizi alikua Omari Suleiman aliyekuwa fundi cherahani na Haruna Taratibu Fundi Mwashi, Public Works Department (PWD).

Job Lusinde na wasomi wengine wa Makerere waliokuwa walimu pale Alliance walijiweka mbali na harakati hizi kwa kuhofia kupoteza kazi zao.

Lakini mimi sikumpeleka huko nilitosheka na kumfahamisha kuwa nimemtaja katika kitabu changu.

Job Lusinde alinijia kama mtu mkimya na mpole jinsi alivyokuwa anazungumza na mimi.

Nilikuwa na nakala ya kitabu hicho katika mkoba wangu nikaufungua nikamkabidhi.

Alinishukuru na nikawaomba niwapige picha ya pamoja wakanikubalia nikawapiga na tukaagana.

Job Lusinde alinijia kama mtu mkimya na mpole jinsi alivyokuwa anazungumza na mimi.

Haukupita muda mrefu Spika Samuel Sitta akafariki, kisha Balozi Job Lusinde na leo Balozi Saleh Rajab Tambwe ametangulia kwa Mola wake.

Tunamuomba Allah amfanyie wepesi Balozi Tambwe katika safari yake hii.

Amin.​

Screenshot_20210125-180306.jpg


Angalia picha: SALEH RAJAB TAMBWE, JOB LUSINDE NA SAMWEL SITTA

Screenshot_20210125-194119.jpg
 
Innalillah wainna ilayh rajiuun....ALLAH amfanyie wepesi amiin.
 
Mzee wetu Mohamed Said naomba uweke picha zako maana ninayo moja tu ukiwa umesimama mbele ya mnara wa Eiffel. Pia ikikupendeza uweke wasifu wako tukujue kabisa legend, kama uzi upo unaojieleza nauomba
 
Poleni sana. Hii trend ya vifo sio ya kawaida. Kuna nini hasa?
 
RIP
kuepuka taharuki na kuleta songombingo hususan wakati huu ambapo misiba imekuwa mingi kama itawapendeza wanafamilia/waleta hanari wangekuwa wanaweka na chanzo cha vifo kama ni ajali, malaria pneumonia n.k.
 
Mzee wetu Mohamed Said naomba uweke picha zako maana ninayo moja tu ukiwa umesimama mbele ya mnara wa Eiffel. Pia ikikupendeza uweke wasifu wako tukujue kabisa legend, kama uzi upo unaojieleza nauomba
T14...
Mimi ni mtu wa kawaida sana sina umuhimu huo unaodhani ninao.

lngia hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com
 
Ahasante Mohamed kwa taarifa hii ya kusikitisha. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu BALOZI SALEH BOI TAMBWE mahala pema peponi.
 
Back
Top Bottom