nimesingiziwa nimefariki wakati nipo kazini.

ambwilikiti

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2014
Posts
204
Reaction score
59
wadau naombeni msaada wakisheria,mimi ninafanyakazi serikalini takriban miaka 7 hv,cha kushangaza mwaka jana walininyima mshahara kwa muda wa miezi mitano na kunifuta kabisa kny payroll baada ya kufuatilia nikaambiwa kwa mshangao na afisa utumishi mmoja pale wizara ya utumishi..."mbona zimetumwa taarifa toka halmashauri yako kuwa wewe si mfanyakazi tena wa serikali kwani umeshafariki dunia miezi mitano iliyopita".Hapo nikashikwa na butwaa na hadi leo nimerudishiwa mshahara lakini sijalipwa mishahara yng ya miezi mitano ya kifo hewa wakati wameshajiridhisha wenyewe kuwa nilikuwa hai na nipo kazini hadi sasa!!!:flypig::flypig:
 
Waambie wakuonyeshe kwanza nakala ya cheti/hati ya "kifo chako", from there utajua pa kuanzia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…