Uchaguzi 2020 Nimesoma ilani za vyama vitatu, ya ACT-Wazalendo ni bora zaidi

Uchaguzi 2020 Nimesoma ilani za vyama vitatu, ya ACT-Wazalendo ni bora zaidi

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2020
Posts
275
Reaction score
802
Nimesoma ilani ya CCM aka Thesis, ya CHADEMA, na ACT-Wazalendo. Kusema ukweli ACT-Wazalendo wamedhihirisha wana wasomi vichwa.

Kwanza wamechambua mapungufu katika utekelezaji wa ilani ya chama kilichotawala 2015/2020 ( performance assessment), harafu wakatoa ahadi zao pamoja na kuonesha ahadi zao zitatekelezwa vipi. Na gharama ya miradi ni shilingi ngapi. ACT-Wazalendo wameainisha mpaka vyanzo vya mapato.

Kingine ambacho kinanifanya nivutiwe na ACT-Wazalendo ni jinsi walivyojipanga, focus, utulivu, na kutumia maneno yenye staha kwenye kampeni.

Hongereni ACT-Wazalendo

Hongereni vichwa wa ACT-Wazalendo. Ningekuwa na uwezo, tungeomba chama kile kitumie ilani yenu. Namaanisha wale wenye Thesis.

Viva Membe, Viva
 
Ingekuwa watanzania tunavipima vyama kulingana na ahadi zao (ilani) ACT-wazalendo ni sehemu sahihi.

Mbaya zaidi na ni ngumu kuamini, kuna watanzania watakichagua chama fulani kwasababu kinanadiwa na wasanii maarufu.
 
Ingekuwa watanzania tunavipima vyama kulingana na ahadi zao (ilani) ACT-wazalendo ni sehemu sahihi.

Mbaya zaidi na ni ngumu kuamini, kuna watanzania watakichagua chama fulani kwasababu kinanadiwa na wasanii maarufu.
Kabisa aisee. Hawa jamaa unaweza kuwapa serikali
 
Anyway, bado hata na hivyo ilani huwa ni proposals zaidi. Kuna sehemu inaitwa utekelezaji.

Mfano tangu 2005 enzi ya kikwete ukijumlisha ahadi za ilani za CCM endapo zingetekelezwa leo tusingekuwa hapa tulipo.

Maana yake ni kwamba ilani haina maana yoyote saa nyingine, jambo kubwa la umuhimu kwenye kampeni ni kuona chama kipi kina dira ya kubadilisha hali fulani ambayo siyo ya kuridhisha kwa wakati huu.

so hapo mimi naona ilani ya Chadema inanguvu sana kipindi hiki kuliko ya CCM na ya ACT kwa sababu imelenge moja kwa moja kutoa solution ya mambo ambayo siyo ya kuridhisha nchi inapitia kwa sasa
 
Ile ilani ya CCM inakazania ndege na meli za mizigo. Haya madubwana yatakausha mzunguko wa pesa sana
Hapo ndo naona wamepotea njia.. nilivomsikia magufuli anazungumzia mambo ya ndege za mizigo, tayari ameniondoa kwenye reli
 
Kweli iko vizuri sana inaonyesha ni namna gani wako makini ni suala la muda tu kinaweza kuja kuwa chama upinzani chenye nguvu. Wasiporuhusu tumbo kuongoza kichwa na mihemko watafika mbali.
 
Mkuu, utapimwa kwa malengo unayojiwekea ndani ya ilani. Kama kuna ya ziada yasiathiri utekelezaji wa malengo yako. Mfano kuna miradi mingi haikuwa kwenye ilani 2015 imeathiri utekelezaji wa malengo mfano kugawa laptop kwa walimu, na kugawa 50 milioni kwa kila kijiji. Hiki ni kipimo cha kufeli. Hatutampima kwa miradi iliyotekelezwa kinyume cha utaratibu.
 
Hakuna ilani nzuri kwa vyama vyote katika uchaguzi wa mwaka huu kushinda ya Chauma,

Naumia sana kuona anaenda kugalagazwa pamoja na ilani iliyoshiba.
 
Kiukweli ACT wana ilani nzuri,tatizo kubwa hawana wanasiasa wanaoaminika has a kwa upande wa bara.Zitto haaminiki anasimamia nini, kote yupo
 
Mimi Asingekuwa Hasimu Rungwe na Ubwabwa wake basi mbadala wake ingalikuwa ni ACT.
 
Back
Top Bottom