Nimesoma vitabu 655 na haya ni mapinduzi makubwa saba yaliyotokea maishani mwangu

Hicho ndiyo wengi wasichokijua. Wanasoma vitabu ili ku tally kwamba amemaliza kusoma na matokeo yake kumbe anazidi kuwa mjinga na msimuliaji.
Hicho kitabu ulichokitaja cha 7 habits of highly effective people mimi ninacho mwaka wa 14 huu bado sijakimaliza, sababu kuna vitu unavisoma, unspaswa kuvielewa kwa kufanya ulinganifu na vingine inabidi kuviishi, inaweza ikakukula zaidi ya mwaka ukiifanyia kazi Chapter moja tu. Lengo la kusoma ni ili kutafuta au kuongeza maarifa ili tufanye maboresho maishani au tuanzishe projects, siyo ili kuwatajia watu idadi ya vitabu ulivyosoma au kusimulia ulicho kisoma.
Kusoma vitabu ni Project, binafsi ninashangazwa sana na huu ukasuku ulioibuka hivi sasa.
 
Kitabu kimoja miaka 14 wewe sio msomaji wala usijitetee kwa hoja ya kufanya kwa vitendo nani alikueleza kusoma kitabu kimoja muda mrefu ndio mtendaji...Hakuna anayesoma vitabu vingi alafu asiwe mtendaji nioneshe mtu huyo.

Wasomaji vitabu Duniani ninaowajua mimi wana record ya kusoma vitabu vingi tu kwa muda mchache ratio ya kawaida kwa msomaji kweli hapungui vitabu 50 kwa idadi mwaka mzima mimi sijaamua serious sana kuanza kusoma ila kwa mwaka jana nimesoma vitabu 6 kwa idadi wewe unayesema kitabu kimoja miaka 15 hakuna mtu timamu atayekuelewa Unless uwe umechanganya baada ya kusema Retain (kurudia kusoma) hapo kweli maana ni jambo la kawaida tu kurudia kusoma kitabu kwa msomaji kawaida ila ukituambia kwamba ndani ya miaka 15 ujamiliza sio unakirudia ni ujakimaliza iyo ni Comedy.

Kusoma na Kutenda
_Kusoma vitabu vingi kwa muda mchache au kusoma vitabu vichache kwa muda mrefu hai guaratee utendaji ya uliyoyasoma kutenda ulichosoma ni mtu mwenyewe ila naamini hakuna mtu mzima aliamua kwa matakwa yake kusoma vitabu serious vingi let say 30 kwa mwaka mmoja alafu asifanyie vitendo NEVER NEVER nina EXPERIENCE na wasomaji na najua nini kina wa drive kusoma.
 
Kuna watu wamenuna ulivyosema ulipata division I point 3.

Na mimi naongezea ni kweli ulipiga one ya 3 Ilboru PCB kisha ukaenda Muhimbili. Wenye roho mbaya wakakusimamisha masomo ukiwa mwaka wa 3 baadaye ukarudi ukamaliza sasa wewe ni Dr. kamili.

WAZIDI KUNUNA SASA!



Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Wengine tunatamani kusoma kuongeza maarifa lkn lugha mtihani
 
Kwa nini hao wenye roho mbaya walimsimamisha peke yake na sio intake yake yote walioingia pamoja ?

Ni kweli alifanyiwa roho mbaya au kulikuwa na kosa amelifanya akatunisha misuli ?

Mimi sijui ila napata tabu sana kuamini kwamba alifanyiwa roho mbaya.

Kuondoa utata aweke sababu ili kuondoa hiyo doubt na asipake watu matope.
 
Mwamba umetisha sana
 
Haiwezi ukawa bilionea, trust me mkuu. Ila nijuacho ni kwamba utakuwa mwingi wa maarifa na labda hekima lwa ajili ya ku motivate waliokata tamaa na wasioona njia.
Mara ya kwanza nilikua kama wewe.
Ataukosaje ubilionea na huku ameshaianza safari ya ubilionea?
 
House of Wisdom Bookshop pako vizuri. Tokea nipafahamu mwaka 2013, pamekuwa kimbilio langu inapotokea nimekosa kitabu fulani Arusha au Mwanza.
 
Safi sana.
 
Utakuta anayesema si vizuri ni ambaye si msomaji. Ni sawa na maskini kukuelezea ubaya wa utajiri. Hivi utamwamini mtu kama huyo?

Kama si msomaji wa vitabu usiupokee ushauri wake.
 
VITABU vinasaidia Sana maana maarifa yalipo katika VITABU yanakujenga na kuishi vizuri na watu kuheshimu kila mtu na Kuacha kulalamika watu ,kuwaongelea watu vibaya na kushukuru kwa kila Jambo.


Katika uchumi PESA unajifunza njia nzuri za kuweka akiba na kujua namna sahihi ya kuwekeza


Kiroho pia unakuwa vizuri kwa kuishi Usafi wa Mwili roho na Matendo


Pia unakuwa unaandika mantiki na kuongea mantiki.
 
Napenda kusoma vitabu.....
Tatizo muda.....ila ndugu iko kama umetudanganya....hasa katika muda.
 
Miaka kumi na nne? Kina kurasa milioni ngapi?

Kama kurasa hazifiki milioni moja, basi ujue wewe ni mvivu uliyepitiliza.

Si lazima uelewe kila kitu kilichopo kwenye kitabu. Ukipata idea moja kwa kila kitabu inatosha sana. Na kama utasoma, tuseme vitabu mia moja katika mwaka mmoja, utakuwa na idea mia moja kwa mwaka mmoja.

Ukizitendea kazi utakuwa bora mara mia kuzidi aliyetaka kukikariri kitabu kimoja.

Na, kitabu utakachokiona ni kizuri sana, unaweza ukakirudia kukisoma mara nyingi kadiri upendavyo na upatapo nafasi. Mimi kuna ambacho katika kipindi cha miaka kumi, nimeshakirudia zaidi ya mara mia, lakini hilo halikunizuia kuendelea kuvisoma Vitabu vingine.

Kama wewe ni msomaji kweli, usikose kuvisoma alau Vitabu hamsini kwa mwaka!
 
Pokea salute yangu Dr!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…