Nimetembelea mfumo wa ukataji ticket ( Online Booking ) wa Mabasi ya Shabiby, Tuwapongeze Developers wamejitahidi

Nimetembelea mfumo wa ukataji ticket ( Online Booking ) wa Mabasi ya Shabiby, Tuwapongeze Developers wamejitahidi

RobyMi

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2012
Posts
848
Reaction score
863
Habari JF,

Nina safari ya kwenda dodoma Jumatatu, leo nikasema niweke ticket in advance kupitia mfumo wa Shabiby wa ukataji ticket, kiukweli kama mdau wa maswala ya technolojia, huu mfumo umekaa vizuri.

Tuwapongeze developers na kampuni nzima ya Shabiby kwa kufanikisha kutengeneza huu mfumo. Mfumo umekaa vizuri sana, user friendly, mobile responsive na kazi unafanya, mara ya kwanza nliona kama propaganda na sikutaka kabisa kuutumia ila leo nimeamini kweli ni mfumo unafanya kazi, nafikiri hasa kwa watumishi wa serikali walio na safari za kila unawasaidia sana

Kuna baadhi ya vitu kidogo, wakati wakiendelea kuufanyia maboresho ningependa kuona vinakuwepo huko mbeleni
  • Uwezo wa mteja kupilia kwa zaid ya mtandao mmoja, kwa sasa ni mpaka uwe na line ya TIGO tu
  • Uwezo wa mteja kukata booking zaid ya siti moja kwa wakati mmoja
  • Uwezekano wa abiria kuwa na account yake mwenyewe, nafikiri kwa wale wasafiri wa kila siku itawasaidia kutokuwa wanarudia rudia information kila wanapokuwa wanafanya booking
  • Kama ikiwezekana kutengeza mobile application, lakini makampuni yaongezeke, Shabiby wanaweza kufanya kazi kama agents wa makampuni mengine ndani ya mfumo wao
Pia kwa hao madeveloper, ningependa kuona baadae huu mfumo unatumika kwa makampuni mengi zaid, sijatembelea sana mifumo ya mabasi mengine, ila kwa sasa nafikiri huu ni moja ya mifumo bora zaid Tanzania kwa online bus ticketing.

Hongeren Shabiby !

Shabiby Online Bus Booking

3.png 1.png
 
iyo ishu bomba sana nikihitaji kuja huko itanibidi kufanya ivyo kwan hawana punguzo kwa sisi tunaofanya booking ya muda mrefu
 
iyo ishu bomba sana nikihitaji kuja huko itanibidi kufanya ivyo kwan hawana punguzo kwa sisi tunaofanya booking ya muda mrefu
Bado sijajua, ila nahakika wahusika wakiona comment yako wanaweza kufanyia kazi
 
Naona kwa sasa wameturahisishia, mpaka kwa sisi watu wa M-Pesa
Tunashukuru.
 
Tahmeed itabaki kileleni. Chili. Isi-okei
 
Huu mfumo ni second to none. Hakuna kwenda stand kuhangaika na udanganyifu
 
Back
Top Bottom